Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameonyesha kukerwa kutokamilika kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha mji wa Njombe licha ya serikali fedha zote za gharama ya ujenzi huo zaidi ya Sh. bilioni 10. 

Ujenzi wa kituo hicho ulianza tangu Desemba 2013 lakini hadi sasa haijakamilika. Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemjia juu mkandarasi aliyepewa kazi hiyo pamoja na upande wa usimamizi wa ujenzi huo na kudai kuwa umechelewa kukamilika kutokana na uzembe wao. 

“Hapo awali kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na MASASI CONSTRUCTION kwa kujenga awamu ya kwanza na ya pili ambapo katika awamu hizo zimekamilika lakini kwa kuchelewa sana na kulazimika kutafutwa mkandarasi mwingine ili akamilishe awamu ya tatu ambayo ni ya mwisho kwa mradi huo,”amesema. 

Amebainisha kuwa awamu ya tatu Halmashauri ya mji wa Njombe wamempata mkandarasi mpya ambaye ni kampuni ya HAINAN INTERNATIONAL na amesaini mkataba mwezi Mei 2018 na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo mwezi Februari 2019. 

Jafo amewaonya wakandarasi ambao wanachukua kazi lakini wanapopewa kazi wanaleta ubabaishaji katika kukamilisha kazi hizo. Amemuagiza mkandarasi huyo mpya kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma bora kama serikali ilivyokusudia. 
Waziri Jafo, kabla ya kutembelea kituo hicho, alisimamia harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule ya sekondari Makoga iliyopo wikayani Wanging’ombe ili iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano hapo mwezi Julai 2018. 

Katika harambe hiyo kiasi cha sh.Milioni 137 zilichangwa na wananchi wa Wanging'ombe na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akisisitiza jambo kwa wakandarasi wapya wanaojenga Kituo cha mabasi cha Mji wa Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha mabasi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akisikiliza taarifa ya ujenzi wa Kituo cha mabasi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akipanda mti wa Matumaini kabla ya Harambee ya shule ya Makoga mkoani Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akiendesha zoezi la Harambee katika wilaya ya wanging'ombe kwa ajili ya sekondari ya Makoga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...