Na Grace Semfuko, Maelezo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imewekeana saini na Kampuni ya Kanton Investment kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata zao la mihogo, ikiwa ni juhudi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuvutia wawekezaji nchini.

Ujenzi wa kiwanda hicho utakaogharimu Dola milioni 10 unatarajia kuchakata tani 200 za mihogo pamoja na kusafirisha tani 400,000 za wanga kutoka katika tani milioni 1.6 za mihogo mibichi itayosafirishwa nchini China.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki Wilayani Handeni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kanton Investment, John Rwehumbiza wakati wa hafla ya utiaji saini wa maktaba wa makubaliano hayo iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali.

Rwehumbiza amesema kampuni hiyo imeanza majaribio ya kununua na kusafirisha nje ya nchi zao la Muhogo na kuonesha kupendwa raia wa China, na hivyo kuahidi kufanya uwekezaji kwa kujenga kiwanda cha wanga na kununua mihogo ya wakulima na kuisafirisha nchini humo.

Aidha ameongeza kampuni yake pia imepanga kutoa elimu kwa wakulima wa zao la muhogo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wa zao hilo ambalo litawawezesha kutoa faida kubwa na hasa ukizingatia walaji wengi wa zao hilo wanatoka nje ya nchi ikiwepo China na Japan.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Mafukwe amesema Ofisi yake itahakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hao ili wafanye kazi katika mazingira wezeshi kama ilivyokusudiwa ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa Wilaya hiyo.
 Mojawapo ya shamba la Muhogo uliostawi katika kijiji cha Kwamsisi Wilayani Handeni kwa ajili ya malighafi itakayotumika katika mradi wa kiwanda cha kuchakata muhogo
 Bw. Sultan Mbuji mkulima wa zao la muhogo akitoka shambani kwake kuvuna zao la muhogo huko Wilayani Handeni 

Katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Mafukwe akikabidhiana mkataba na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Kanton Investment Bw. John Rwehumbiza mara baada ya kusainiwa huko Handeni Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...