Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mshtakiwa Habinder Seth kuonana na mke wake anapokuwa mahabusu gerezani.

Ruhusa hiyo imetolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi ya utakatishaji dhidi ya Habinder Seth na James Rugemalira ilipokuja mahakani hapo kwa kutajwa.

Mapema, Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai aliieleza Mahakama kuwa, upelelezi wa ndani katika kesi hiyo umekamilika walikuwa wanafanya mawasiliano na nchi husika na katika mawasiliano hayo baadhi yamefanikiwa. Hivyo akaomba muda ili waweze kukamilisha upelelezi.

Aidha alidai kuwa, wamepokea taarifa kutoka kwa jopo la madaktari waliomfanyia uchunguzi Seth na wameelezwa kuwa mshtakiwa huyo hana shida isipokuwa anatakiwa kutolewa balloon tu lililopo tumboni mwake hivyo wanasubiri daktari wake kutoka Afrika Kusini afike kama matakwa ya mshtakiwa.

Kabla ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, Wakili wa utetezi, Dorah Malaba aliiomba mahakama iwapatie kibali cha kumruhusu mke wa mshtakiwa Seth, kwenda kumuona mume wake gerezani na kudai kuwa walipeleka barua kwa mkuu wa magereza kwa ajili ya kupata kibali hicho lakini ilishindikana.

Pia ameuomba upande wa mashtaka wajitahidi kukamilisha upelelezi ili haki iweze kutendeka.Aidha wakili utetezi wa Rugemalira, Didas Respicious alidai, "Ni mwaka sasa washtakiwa tangu wafikishwe mahakamani upelelezi bado, tunaomba haki itendeke kwa kuleta ushahidi kwani washtakiwa bado hawajapatikana na hatia, ili tujue kama wateja wetu wanashtakiwa au la.

Kutokana na taarifa ya Seth na mkewe, Hakimu Mashauri amesema" Hapaswi kuingikia taratibu za magereza lakini mshtakiwa anahaki ya kuonana na mkewe, hivyo naruhusu mshtakiwa aonane na mke wake. " amesema Hakimu Shahidi.Washtakiwa hao, wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 na Sh.bilioni 309.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 21mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...