Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa Dini nchini kuunga mkono azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda.

Makamu wa Rais ameyasema haya wakati wa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora. Makamu wa Rais amesema hivi karibuni Serikali imepitisha mabadiliko na mpango mpya wa uwekezaji Tanzania.

Makamu wa Rais amesema kuwa kudumisha Amani na usalama ni jukumu la wote “ Endeleeni kuhubiri Amani na kwa upande wa Serikali niwahakikishie Watanzania Wote kwamba Amani na Usalama ni kipaumbele chetu hatuta vumilia kumstahimilia mtu yeyote yule ambaye ana lengo la kuharibu Amani ya Tanzania hatutamvumilia tutamshughulikia ipasavyo”

Makamu wa Rais amesema “Tukosoeni pale tunapokosea nasi tunawaahidi tutarekebisha na twende mbele kwani Mwalimu Nyerere alituambia kuongoza nikuonyesha njia na katika kuonyesha njia lazima ukubali kukosolewa nasi tunakubali kukosolewa hilo nalo ni jukumu la utumishi wa kiroho kwa hiyo endeleeni kutukosoa kwa ile lugha ambayo tutafahamiana”

Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Taasisi za dini katika masuala ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii. Makamu wa Rais amelishukuru na kulipongeza Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa mchango wake mkubwa unatoa katika nchi yetu hususani katika Nyanja za Elimu, Huduma za Afya na Maji.

Nae Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Fredrick Shoo alisema kuwa wameona jitihada za Mheshimiwa za Rais na wataendelea kumuunga mkono na wapo pamoja kushirikiana na Serikali kwa nia njema kabisa. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Mch. Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Newton John Maganga, mkoani Tabora leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kuwasili kwenye Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na kumuweka Wakfu na kumuingiza kazini Askofu Mteule Mch. Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Newton John Maganga, mkoani Tabora leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais akisalimiana na Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser wakati wa ibada ya ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kamba kama ishara ya zawadi ya ng'ombe wa maziwa kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Fredrick Shoo wakati wa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maaskofu wote kutoka Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Kuzindua Dayosisi ya Magharibi Kati na Kumuweka Wakfu na Kumuingiza kazini Askofu Mteule Mchungaji Dkt. Isaac Kissiri Laiser na kuingizwa kazini Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Newton John Maganga katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tabora. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...