Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro ameipongeza mahakama ya Tanzania kwa utekelezaji wa miradi ya mahakama kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya ujenzi wa bei nafuu ya mradi wa Molandi.

Pia Okoro ameipongeza mahakama kwa kuzingatia uwiano wa jinsia mahakamani katika utekelezaji wa majukumu kwani ameona kutoka ngazi za juu hadi ya chini wanawake wako wengi, 

Okiro amesema hayo leo Juni 8,2018 wakati anatembelea Mahakama ya Mwanzo na ile ya Wilaya ya Kigamboni iliyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo alishuhudia majengo na kupewa maelezo mbali mbali yanayofanywa na mahakama za Tanzania. Ikiwemo mahakama inayotembea (Mobile Court).

Amesema taarifa za ujenzi wa majengo hayo ni za mfano wa kuigwa na zinapaswa kuwa mfano wa nchi nyingi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwani majengo hayo ni mazuri na yanakidhi thamani ya fedha.Amesema, taarifa ya namna ya mfumo wa mawasilisho na ujenzi na jinsi miradi hiyo inavyofanya kazi,ni mfumo mzuri na ni kitu cha kuigwa kwani inaonyesha wazi ni jinsi gani jengo lilivyo na mfumo mzuri.

"Nimefurahi sana, miradi imejengwa kwa mfumo mzuri, majengo nilikuwa nikiyaona kwenye documents tu lakini sasa hivi nimeyaona, yanakidhi vigezo na thamani ya pesa", amesema Okiro.

Kabla ya kuongea hayo, makamu wa rais huyo, alipata nafasi ya kusikikiza taarifa (Presentation) kutoka kwa Mhadhiri Mwandamizi wa Mfumo (Court Mapping) kutoka chuo cha Ardhi Job Chaula amesema, katika mahakama hiyo, wameweka mifumo ya mawasiliano ya kutoa taarifa mbali mbali za mahakama itakayomuwezesha mwananchi kufuatilia kesi bila ya kufika mahakamani, na vile vile ramani ya kufika mahakamani hapo kutokea mahali popote.
Mhadhiri Mwandamizi wa Mfumo: Court Mapping kutoka chuo cha Ardhi Job Chaula, akieleza jinsi mfumo wa kutoa taarifa mbali mbali za mahakama una vyofanya kazi katika Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni kupitia mradi wa Court Mapping. 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk. Daniel Mbisso, akieleza jinsi teknolojia ya Moladi ilivyotumika kujenga majengo mbalimbali ya Mahakama na kufanikisha kwa mafaniko makubwa mahakama zaidi ya tano zilizojengwa kwa muda mfupi na garama nafuu.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro (katikati) aliyevaa miwani akiwa katika Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro kulia akizungumza na wadau mbali mbali wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi. Pembeni yake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...