Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.

Jenerali Mabeyo ametoa ushauri huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Juni 07, 2018.

Mabeyo amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya kuajiriwa  .

“Vijana tunaowachukua JKT ni kwa ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili hata kijana akikosa nafasi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza kurudi kijijini akafanya vitu vya maendeleo, mimi nadhani watu wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT lazima aajiriwe,  ipo haja ya kubadili mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo

“Jeshi linachukua vijana elfu ishirini kwa mafunzo, wanaochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama hawazidi vijana 2000 sasa hawa wengine 18,000 wanaenda wapi, kama mawazo yatakuwa ni kwenda JKT ili kuajiriwa hatutafanikiwa lakini kama watakwenda JKT kujifunza stadi za kazi kuwasaidia ili ziwasaidie kujiajiri na kubadili maisha yao tutafanikiwa sana” alisisitiza.
 Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini kwake Juni 07, Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akitoa taarifa fupi ya mkoa kwa Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo(kulia)  wakati alipomtembelea ofisini kwakeJuni 07, 2018 Mjini Bariadi na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi  walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa mkoa wa   Simiyu, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi  walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka  Mjini Bariadi, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
 Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kumaliza mazungumzo  na viongozi hao , Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  wakiteta jambo baada ya Mkuu huyo wa Majeshi kuzungumza na viongozi Mkoani humo Juni 07, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...