Na Bashir Yakub. 

Wapo watu wana matatizo na wanahangaika kupata msaada wa bure wa kisheria lakini hawajui waanzie wapi,wafanye nini ili kupata huduma hii. Taratibu zipo, na unaweza kupata wakili wa kusimamia kesi yako bure bila malipo kupitia utaratibu wa msaada wa kisheria. Unaweza kupata uwakilishi huu katika kesi zote yaani zile za jinai pamoja na zile za madai. 

Tunapoongelea za jinai tunamaanisha zile kesi za kuua,kubaka, kupiga,kutukana nk, na tunapoongelea kesi za madai tunamaanisha zile za ardhi kugombea mali, mirathi, ndoa, mikopo,watoto malezi, talaka, nk. 

Kwahiyo pote kwenye jinai na madai unaweza kupata uwakilishi wa bure wa Wakili. Utasimamiwa kesi yako mwanzo hadi mwisho bila kuhitaji kulipa gharama yoyote. Na msaada wa kisheria unaweza kuwa wa uwakilishi kwa maana kuwa wakili utakusimamia mahakamani au unaweza kuwa wa ushauri tu bila kuhusisha mahakama au vyote kwa pamoja. 

Lakini yafaa tufahamu kuwa sio watu wote wanaweza kupata msaada huu. Makala yataeleza utaratibu wa kupata msaada wa kisheria bure halikadhalika ni watu wa aina gani wanaweza kupata msaada huu.

1.WANAOSTAHILI KUPATA MSAADA WA KISHERIA BURE. 

i)Watu wasiojiweza kabisa kifedha. 
ii) Wanawake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimefikia hotelini kwa bahati mbaya pesa imeisha na siku za kukaa zimezidi hivyo gharama zimekuwa kubwa na sina ya kulipa. Hivyo hoteli inanidai na wana mpango wa kunipeleka police. Sheria ikoje hapo? Nipelekwa police, nachukuliwa hatua zipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...