BENKI ya Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB) imetanua wigo wake kwa kuzindua huduma ya Mwalimu Bank Wakala itakayowawezesha Watanzania na wateja wa benki hiyo kupata huduma za benki hiyo kuwa karibu katika maeneo yao wanayoishi au kufanyia kazi.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mwalimu Bank Wakala mkoani Tanga juzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Mwalimu Mwalimu Commercial Bank Plc, Ronald Manongi amesema benki yake imeingia kwenye makubaliano ya kimkakati na Maxcom Africa Plc kupitia mawakala wa Maxmalipo.

Amefafanua lengo ni kuwawezesha wateja wa benki hiyo kuweza kunufaika na benki yao kwa kupata huduma kwa urahisi, haraka na unafuu."Benki yetu ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa tunasogeza huduma zetu karibu zaidi na wananchi popote pale walipo. "Nia ni kuhakikisha kuwa mtanzania popote alipo aweze kupata huduma za kibenki ili kwa pamoja tuweze kukuza uchumi wa nchi yetu, "alisema.

Manongi amesema kuwa benki yao imehakikisha kuwa inaendelea kuwa bega kwa bega na wateja wake kupitia zaidi ya mawakala 10,000 wa Maxmalipo walioenea katika maeneo mbalimbali nchini. Ameongeza wateja wa Mwalimu benki watapata huduma mbalimbali kama kuweka fedha kwenye akaunti zao, kutoa fedha ikiwa ni pamoja na mishahara kwenye akaunti zao, kuangalia salio na taarifa fupi, malipo ya luku, maji na muda wa maongezi.

“Tumejipanga katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu,hivyo kwenye kila huduma tunayoitoa, kwanza tunaangalia mteja wetu anataka nini, ndipo kupitia timu yetu tunabuni njia sahihi yenye ufanisi katika kukidhi mahitaji ya wateja wetu,amesema. Aidha ameongeza wana shauku ya kuona wateja wao wanafanikiwa na wanaamini wateja wakifanikiwa na benki pia itafanikiwa. “Tutaendeleakuja na ubunifu mbalimbali wa kiteknolojia ili kuzidi kurahisisha huduma kwa wateja wetu,"amesisitiza.

Uzinduzi wa Mwalimu Bank Wakala ulifanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo.
   Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa kampuni ya Maxcom Afrika Plc,  Gasper Mrosso (kulia), akimuelekeza mmoja ya wanahisa wa Benki ya Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Handeni (CWT), Hamisi Ngomero  jinsi ya kutumia mashine maalum za POS ili kuweza kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia huduma ya MCB Wakala wakati wa uzinduzi wa rasmi wa MCB Wakala uliofanyika pamoja Mkutano Mkuu wa pili wa Wanahisa wa benki hiyo mjini Tanga mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commecial Bank,   Ronald Manongi na Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Afrika Charles Natai.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Mwalimu Commecial Bank Plc,  Ronald Manongi, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya MCB Wakala uliofanyika pamoja na Mkutano Mkuu wa pili was Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Tanga mwishoni mwa wiki. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Commecial Benki  Ronald Manongi (kushoto) akishuhudia mteja wa benki hiyo ambae pia ni Katibu wa Chama cha Walimu Handeni (CWT), Hamisi Ngomero (wa pili kushoto), akipata hutuma kupitia MCB Wakala huduma iliyozinduliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa pili wa Wanahisa wa benki hiyo mjini Tanga hivi karibuni. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa kampuni ya Maxcom Afrika Gasper Mrosso,  Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Afrika Plc, Charles Natai na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Ubunifu wa Maxcom, Deogratius Lazari.  
  Baadhi ya wanahisa wa benki hiyo wakihudhuria Mkutano wao Mkuu wa pili wa Mwaka mjini Tanga hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...