THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NAIBU WAZIRI MAVUNDE ABARIKI SAFARI YA WAPANDAJI WA MLIMA KILIMANJARO KUTOKA GEITA GOLD MINING (GGM) KWA LENGO LA KUCHANGISHA FEDHA ZA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

ZAIDI ya Sh Bilioni 20 zimekusanywa kutoka kwa mashirika 40 yasiyo ya kiserikali pamoja na taasisi mbalimbali za serikali kwa ajili ya kusaidia katika kampeni za kupambana dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi ambapo tayari Mamilioni ya watanzania wamekwisha nufaika nazo.

Fedha hizo zimekusanywa kampuni ya Kuchimba dhahabu ya Geita (GGM) kupitia changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro, ijulikanayo kama “Kili Challenge” tangu mwaka 2001 ilipoanzishwa ,mwaka huu ukiwa mwaka wa 17 ikishirikisha washiriki 70 watakao shiriki kupanda Mlima huku wengine wakizunguka mlima huo kwa kutumia Baiskeli .

Akizungumza wakati wa Hafla ya kuwaaga washiriki wa Programu ya Kili Challenge 20018 iliyofanyika katika lango la kupanda Mlima Kilimanjaro la Machame ,Makamu wa Rais wa GGM, Simon Shayo amesema Progaramu hiyo imepanua wigo wa kusaidia Taasisi zinazojikita kuhudumia wachimbaji wadogo wadogo pamoja na maeneo ya wavuvi ambako tafiti zinaonyesha wako kwenye mazingira hatarishi ya kuambukizwa VVU.

“Kila siku na kila mwaka ,tukio hili la hisani linaendelea kuwa na matokeo makubwa kwa jamii inayotuzunguka ,ninayo furaha leo kutagaza kwamba kupitia Kili Challenge tumeweza kuchangisha zaidi ya Bilioni 20 .”alisema Shayo.

Alisema fedha hizo zimekusanywa kutoka katika Mashirika 40 yasiyo ya kiserikali (N.G.O,S) pamoja na taasisi mbalimbali za serikali kupitia Tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo watanzania zaidi ya Milioni moja wamenufaika nayo.
 Mgeni Rasmi katika tukio hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde akikabidhi Bendera kwa washiriki wa changamoto hiyo kwa njia ya kuzunguka mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavundeakijaribu kuendesha Baiskeli kuashiria uzinduzi wa Changamoto ya kuzunguka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baikeli.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavundeakishirikia zoezi la Kupanda Mlima Kilimanjaro kuashiria mwanzo wa safari ya wapandaji 40 wanashiriki zoezi hilo. 
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah ni miongoni mwa washiriki walioanzisha safari hiyo.