Na John Nditi, Morogoro

POLISI mkoani Morogoro inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu mwanamke aliyejifungua mtoto wakati akiwa njiani kupelekwa Kituo cha Afya Mang’ula, wilaya ya Kilombero mkoani humo mara baada ya kutolewa mahabusu ili kubaini kama kuna uzembe wowote umefanywa na watendaji ama askari na ikibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Mugabo Wekwe alisema hayo katika taarifa yake kwa waandishi wa habari juu ya tukio la kujifungua mtoto njiani mwanamke Amina Rafael Mbunda (27) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa , Tarafa ya Mang’ula , wilayani Kilombero , mkoa wa Morogoro.
Alisema , Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio la mwanamke huyo aliyefikishwa katika kituo cha Polisi Mang’ula kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi kisha kujifungua akiwa njiani kuelekea katika Kituo cha Afya Mang’ula.
Alisema , Mei 31, mwaka huu ilifunguliwa kesi ya wizi wa samani mbalimbali zenye thamani ya Sh 1,040,000 katika kituo cha Polisi Mang’ula kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro zilizoibwa kwa vipindi tofauti katika karakana ya Joseph Mdee iliyopo maeneo ya Posta Mang’ula .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo alisema, baada ya tukio uchunguzi ulianza mara moja na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja alitwaje Ridhiwani Athuman na kukiri kuiba kisha kuwauzia watu mbalimbali akiwemo Abdallah Mohamed Mrisho (40) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa Tarafa ya Mang’ula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...