Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.
MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amemshukuru Rais na viongozi wote ambao wanashiriki katika ujenzi wa taifa.

Pia amehaidi kutoa ushirikiano wakandarasi ili waweze kutekeleza miradi na amezuia malori kupita katika kijiji cha Kitoga kwa muda wa miezi miwili hadi ujenzi wa daraja hilo utakapokamilika. 

Akizungumza leo Sanga pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Julai 12 kuupokea Mwenge wa uhuru ambao utafungua miradi mingi ya kimaendeleo.

Kwa upande wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika ziara yake katika jimbo la Mkuranga ameendelea kukagua ujenzi wa barabara katika kata za Tambani, Mipeko, Mkuranga, Kimanzichana, Mkamba na kata ya Kisegese.

Ulega ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kukagua ukarabati wa barabara mara baada ya mvua kunyesha, na amesema kuwa wamekagua katika kata mbalimbali na wameridhishwa na utendaji kazi unaofanywa na wakandarasi katika kutekeleza mradi huo kwani fedha iliyotolewa na kinachofanyika vinawiana.

Aidha Ulega amemshukuru Rais Magufuli kwa kuangalia mahitaji ya wananchi na kuyafanyia kazi na kuahidi kuwa kama wasaidizi wake watamuunga mkono katika kulipeleka taifa katika hali nzuri ya uchumi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu.

Amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo ili kuwarahisishia shughuli mbalimbali na kuweza kudumu kwa matumizi ya kizazi kijacho.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega akishiriki ujenzi wa daraja katika kijiji cha Mipeko katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akishiriki ujenzi wa daraja katika kijiji cha Mipeko ,kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali,iliyo fanyika leo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mihekela alipo tembelea na kukagua barabara ya kijiji hicho,ambapo alimuomba Meneja wa TARURA kujenga barabara hiyo kwa kiwango chenye ubora na kuhakiksha sehemu korofi zinaimarishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...