Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Mamamlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwana, Saada Omar Ally (kushoto) kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada huo.


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, limetoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu kwa watoto waishio katika mazingira magumu ili kuwawezesha kufurahia Sikukuu ya Eid.

Msaada huo umetolewa kwa Vituo vya DMI kilichopo Kibamba Kibwegere chenye watoto 60 na Kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti chenye watoto 85 vyote vikiwa jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba, Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi amesema, Shirika lake linatekeleza kikamilifu wajibu wa Taasisi za Umma na Binafsi wa kutoa sehemu ya mapato yake kwa ajili ya ustawi wa Jamii na kuleta unafuu kwa maisha ya watu wanao wazunguka.

“Huu ni utaratibu wetu wa kila mara hali inaporuhusu, tunajitoa kwa ajili ya wahitaji na hasa watoto wa naoishi katika mazingira magumu ili kuwapa matumaini ya kujiendeleza ki-elimu na kujitegemea ili kuwa raia wema wasiku za baadae. Tuna waomba Watanzania watuunge mkono kwa kutumia huduma zetu ili kutupa nguvu ya kuendelea kusaidia jamii kwa matendo mema kama haya,” alisema Ndugu Thom Mushi.

Wakishukuru kwa misaada hiyo, Viongozi wa vituo vyote viwili wameiomba TTCL na Taasisi nyingine kuendelea kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu na hasa watoto wenye ndoto nyingi za kubadili hali zao za maisha na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada mmoja wa watoto (kushoto) wa kituo cha DMI inachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata cha Kibamba, jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Sista Makrina Kapinga (kushoto) mlezi wa Kituo cha watoto yatima cha DMI kinachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata cha Kibamba, jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia),
akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Mamamlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwana, Saada Omar Ally (kushoto) kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...