Na Abdullatif Yunus wa  Globu ya Jamii, Kagera
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  wa Kagera kupitia Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kagera imezindua rasmi pasipoti ya kielektroniki kwa wananchi na wakazi wa Mkoa huo. Tayari pasipoti hizo zimeanza kutolewa tarehe Junin7, 2018 katika hafla  iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, maafisa kutoka jeshi la Uhamiaji, viongozi wa dini, wananchi na wadau wa Idara ya Uhamiaji katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.
Katika hotuba yake Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu iliyotolewa na mwakilishi wake Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Mh. Deodatus Kinawiro, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma hii ya pasipoti huku akitaja faida lukuki za kuwa na pasipoti ya aina hii. miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kukidhi matakwa ya usalama wa Nchi, na pia kukidhi viwango vinavyopendekezwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia mambo ya anga.
Kwa mujibu wa idara ya Uhamiaji mpaka sasa tayari Jeshi la Uhamiaji limekwishatoa jumla ya pasipoti 17,598 zikiwemo pasipoti za kawaida, Utumishi, Diplomasia, na Diplomasia maalum tangu zoezi hili lilipozinduliwa Rasmi mapema Januari 31 mwaka huu, na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
​Muonekano wa viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga, katika uzinduzi wa pasipoti ya kielektroniki Mkoani Kagera m ​apema Juni 8, 2018.
Kamishna wa pasipoti na Uraia afande Gerlad Kihiga amesema katika hafla hiyo kwamba pasipoti hiyo imetengenezwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu na haiwezi kugushiwa kitrahisi kwani ina kifaa maalumu ndani yake hivyo itamsaidia msafiri  kutumia E-gates pasipo kuweka msongamano, ikiwa na mfanano wa pasipoti nyingine za Afrika mashariki hivyo unaweza kupata usaidizi ubalozi wowote  katika nchi wanachama, na huku tahadhari ikitolewa kwa wale ambao huwasaidia raia ambao si watanzania kupata pasipoti, kwa atakaebainika pasina kujali ni atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa wale wanaotumia simu janja tayari ipo app ya pasipoti ambayo mwananchi yeyote anaweza kupakua app hiyo katika simu yake na kujaza taarifa zake, au kuangalia taarifa zake.
 ​Sheikh wa Mkoa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta akiomba dua wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.
 Askofu Msaidizi Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini akiomba sala wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.

  Kamishna wa pasipoti na Uraia afande Gerlad Kihiga akikabidhi pasipoti ya kwanza Kagera kwa Mkuu wa Wilaya Mh. Deodatus Kinawiro kwa niaba ya mgeni rasmi katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Mh. Deodatus Kinawiro akimkabidhi pasiposti Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bukoba Ndg. Zachwa katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba akikabidhi Pasipoti kwa Askofu Mkuu wa jimbo la Bukoba Desderius Lwoma katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba. 
Picha na Abdullatif Yunus wa  Globu ya Jamii, Kagera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...