Na Abel Daud,Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga ametoa mwito kwa wajasiriamali mkoani Kigoma kuyatumia kwa vitendo mafunzo wanayopata ya stadi za biashara na ujasirimali kwani ndiyo njia pekee itakayowawezesha kukua katika shughuli zao.

 Anga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wajasirimali kutoka Wilaya hiyo yanayoendeshwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC).

Anga amesema kuwa mafunzo yanayotolewa kuhusiana na kukuza mitaji,utafutaji wa masoko, uboreshaji wa bidhaa na biashara za kuvuka mipaka ya nchi ni mambo ambayo wajasiriamali wakiyatumia ni wazi shughuli zao zitakuwa na mafanikio makubwa.

Pia amesema kuwa bado wajasiriamali wengi wanazalisha bidhaa zao katika viwango visivyozingatia ubora vikiwa na uzalishaji mdogo mambo ambayo yanakwaza wajasilmrimali wengi kukuwa katika shughuli zao.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa TIC Kanda ya Magharibi, Innocent Kahwa amesema lengo la mafunzo yanayotolewa kwa wajasirimali yanalenga kuwafanya wapate faida kwa bidhaa wanazozalisha lakini pia kuwafanya wapanue shughuli zao na kuwa  na mafanikio zaidi katika shughuli wanazozifanya.

Kahwa amesema kuwa msingi mkubwa wa mafunzo yanayotolewa kwa wajasiriamali ni kuwafanya kujua sheria na taratibu zinazoongoza shughuli zao, kujua teknolojia kuwarahisishia shughuli zao lakini pia kujua utawala wa miradi na biashara hasa inapoanza kuwa mikubwa.
Meneja wa Kanda ya Magharibi Innocent Kahwa akitoa mada kwa wajasiriamali mkoani Kigoma.
Baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa kigoma wakisikiliza mafunzo kutoka kwa Meneja wa TIC Kanda ya magharibi.
Afisa ufundi wa Sido Kigoma Alexander Mpuya akitoa mada kwa wajasiriamali wa Mkoa wa kigoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...