Na Dotto Mwaibale

WANAMUZI walio wanachama wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) wiki ijayo watatembelea Bunge kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Umoja huo, Dk.Donald Kisanga alisema kwa umoja huo kwao ni fursa kubwa ya kutembelea Bunge."Kwetu sisi Tamufo kutembelea Bunge ni fursa kubwa na tunaenda kuona jinsi Bunge linavyofanya kazi yake" alisema Kisanga.

Kisanga alisema msafara wao utaondoka jijini Dar es Salaam Juni 23 na Bungeni watakuwepo Juni 25 mwaka huu na mwenyeji wao ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe.

Kisanga aliyataja baadhi ya makundi ya wanamuziki watakaokuwepo kwenye msafara huo kuwa ni wanamuziki wa dansi ambalo litaongozwa na Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kik na Hamza Kalala.

Alitaja kundi la muziki wa Injili kuwa litaongozwa na Stella Joel na Emanuel Mbasha wakati Bongo Fleva litaongozwa na Witness Kibonge Mwepesi huko taarabu likiongozwa na Sizer Masogelo na Muziki wa Asili likiongozwa na Grace Kayinga.Katibu wa Tamufo, Stellah Joel alisema wanamuziki kutoka mikoa yote waliotayari watakuwepo kwenye msafara huo.
Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tamufo, Morocco Dar es Salaam jana wakati wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja huo pamoja na safari ya baadhi ya wanachama wa Tamufo kwenda Bungeni Dodoma.
Mhandisi Abdallah Ally kutoka Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
Mwanamuzi mahiri Kitenzogu Makassy, akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki Hamza Kalala.
Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...