Na Frankius Cleophace Tarime.

Wasichana 40 kutoka katika kata tofauti Wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya uelimishaji rika katika Maeneo wanayotoka kwa lengo la kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto zake ikiwemo kupata Elimu.

Sarah Bedah ni Afisa Mawasiliano kutoka Shirika la Msihana Initiative lililopo Jijini Dar Es Salaam, amesema kuwa wao kama Shirika kwa kushirikiana na Shirila la ATFGM Masanga lililopo Tarime wameamua kutoa Elimu hiyo kwa lengo la kuwajengea Uwezo wasichana hao ili kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha Elimu ya kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya amesema kuwa wao kama shirika wameamua kutoa Pia Mafunzo hayo kwa wasichana ambao wamekeketwa tayari na ambao hawajakeketwa ili kuzidi kuwaelimisha Wasicha ambao hawajakeketwa ili wasikeketwe.

Pia Mgaya ameongeza kuwa licha ya kutoa Elimukwa Wasichana hao bado wanazunguka na wazee wa Mila Muungano wa Koo12 kwa lengo la kutoa Elimu kwa jamii ili kuondoa Ukeketaji ikiwa ni pamoja na Kupiga Vita Miiko ambayo inakandamiza Mtoto wa kike ambaye hajakeketwa ili asitengwe Kwenye Jamii.

Aidha Washiriki wa Semina hiyo ya Siku mbili wamesema kuwa Elimu watakayopewa itakuwa chachu kwao na kuitumia Vyema kwa lengo la kukomboa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Naye Mratibu wa Huduma ya Afya ambaye pia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo Abel Gichaine amesema kuwa baada ya kutoa Elimu kwa jamii endepo itakiuka lazima Sheria itumike ili kuwatia hatiani wale ambao watakao keketa Msichana kwani Mwaka huu unaogawanyika Kwa Mbili wenda koo Nyingi za kabila la Wakurya Wilayani Tarime zikakeketa ili kutimiza Mila zao.

Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga Tarime ambao wanapiga Vita Ukatili wa kijinsia akitoa Somo kwa Mabinti hao ambao baadhi yao wamekeketwa na kuolewa katika Umri Mdogo wakipewa Elimu ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuopiga Vita Ukaili Maeneoo wanayotoka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...