Na Frankius Cleophace, BUTIAMA

Wazee wa Mila Muungano wa koo 12 kabila la Wakurya kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga Tarime, wameendelea kutoa Elimu ya Kupinga suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike kwa lengo la Kumnusuru ili atimize ndoto yake ya kupata Elimu na kutimiza Serikali ya Viwanda.

Wazee hao Muungano wa Koo 12 wamezungukia Koo 12 Wilayani Tarime kwa Kutoa Elimu ya kupinga Ukeketaji huku wakitoa Matamko ya Kuondoa Miiko ambayo imekuwa ikikandamiza Mtoto wa kike ambaye hajakeketwa kupitia Mikutano ya hadhara lengo  ikiwa ni kufikisha Ujumbe.

Licha ya kutoa Elimu hiyo sasa wazee hao wameamua kwenda Wilaya ya Butiama kwa lengo la kufikisha ujumbe huo uliokusudiwa, lengo ni kunusuru Mtoto wa kike.

Akitoa Elimu hiyo Mwita Nyasibora ambaye ni Katibu Msaidizi wa koo hiyo amesema kuwa ,Koo ya Bukenye ni kubwa imesambaa mpaka Wilaya ya  jirani ya Butiama, hivyo wameona ni vyema kufikisha Elimu hiyo ili wasije kukiuka na kukeketa Mtoto wa kike kwa kuwa wazee tayari wamekataa Ukeketaji.

“Sisi kama Wazee Muungano wa Koo12 tumeisha kataa Ukeketaji na Koo itakayokiuka iwajibishwe yenyewe” alisema Mwita.

Mmoja wa wazee wa Mila ametoa ushuhudi jinsi gani Mwanamke zamani alivyokuwa akinyanyaswa wakati mwingine kukeketwa wakati akijifungua jambo ambalo lilikuwa linamwongezea Uchungu mara mbili na kuendeleaza Ukatili lakini kwa sasa wazee hao wameona hakuna faida ya kukeketaji bali hasara ndo nyingi kuliko faida.

Mwenyekiti wa kijiji cha Buswahili Wilaya ya Butiama,Wambura Mwema amesema kuwa kuna haja kubwa ya Wazee hao wa Mila kula kiapo kuhusu Matamko yao ili atakayekiuka ka kukeketa Mtoto wa kike achukuliwe hatua peke yake huku akisema kuwa Serikali inaungana na wazee hao kutokomeza Ukeketaji.
Picha ya Pamoja Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Marea na Koo ya Bukenye Wilayani Butiama baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika kijiji cha Kongoto Kata ya Buswahili Wilayani Butiama lengo ni kuzungumzia Mikakati ya Kupiga Vita Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Katibu Msaidizi wazee wa Mila Muungano wa Koo12 ,
Mwita Nyasibora 
akitoa Elimu kwa wazee hao juu ya madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa kike, ambapo amesema kuwa Wilaya ya Tarime wamezunguka na kutoa Elimu hiyo kwa jamii,hivyo wameamua kufikia Koo ya Bukenye ambayo inaenda mpaka Wilaya ya Butiama.
Mwenyekiti wa Muungano wa wazee wa Mila kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Mara,Nchagwa Mtongori  akijibu baadhi ya Maswali katika kikao hicho likiwemo suala la kutokomeza Wizi wa Mifugo na Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
wazee wa Mila wakiwa katika Kikao cha pamoja

 Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Wilaya ya Butiama 
Werema Osombe 
akiomba aWazee hao kupiga Vita suala la Wizi wa Mifugo ambayo inaibiwa kutoka Wilayani humo na kupelekwa Tarime.
Baadhi ya Wazee wa Mila  wakiwa katika Kikao cha pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...