Chachu ya ukuaji wa uchumi jumuishi Tanzania. 

Benki ya Stanbic Tanzania imezindua kampeni maalumu kwa ajili ya chata yake, yenye kauli mbiu isemayo “Zaidi ya Benki”, ikijitofautisha na taasisi nyinginezo kwa kuwa benki yenye kugusa wateja wake kwa kutoa huduma na bidhaa zenye kuwezesha wateja hao pamoja na watanzania kwa ujumla kufikia malengo yao ya kimaisha.

"Nia na madhumuni ya kampeni hii ya 'Zaidi ya Benki' ni kudhihirisha mchango wetu katika kuboresha maisha ya watu na ya jamii kwa ujumla; mara nyingi watu wanapofikiria benki, huwa wanawaza miamala ya kifedha tu, huku wakisahau kinachojiri baada ya mteja kuondoka na fedha zake," alisema Bi. Desideria Mwegelo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Stanbic Tanzania.

"Sisi hapa Stanbic, tuna desturi ya kufikiria yanayotokea kabla na baada ya miamala kufanyika. Tunaamini kwamba kila tunachofanya hata kiwe kidogo vipi, kina athari katika maisha ya mteja wetu kwa namna moja au nyingine, na ndio sababu huwa tunamfikira mteja katika kila tunachokifanya na kuhakikisha tunaongeza matokeo chanya,” aliendelea kusema.

Kwa mfano, tunaposhiriki katika miradi ya kuleta umeme katika jamii, kwa namna nyingine tunakuwa tumewezesha ukuaji wa viwanda, elimu na fursa nyinginezo zitokanazo na kuwepo kwa umeme.Hali kadhalika kupitia mikopo ya nyumba, watu wanawezeshwa kumiliki nyumba ambazo familia zao hazitokaa zisahau.

Tanzania imesheheni jamii ya vijana wenye jitihada, akili na nguvu, na wenye kutafuta fursa za kujikwamua na kujiendeleza kimaisha kwa kila hali, benki ya Stanbic inataka kuwa sehemu ya jitihada hizo katika kufanikisha ndoto zao na za familia na jamii kwa ujumla.

'Kama wanachama wa Standard Bank Group yenye historia ndefu ya zaidi ya miaka 155 na kuwepo katika nchi 20 barani Afrika, tunaelewa changamoto, tamaduni na watu wa bara hili. Sisi ni zaidi ya benki,’ alisema Bi. Mwegelo. 'Stanbic inahamasishwa na vijana wa kitanzania wenye shauku ya kutumia fursa lukuki zilizopo nchini kwa kutumia ubunifu na mawazo mbadala. Tunataka kufanikisha ndoto zao za kufikia mafanikio ya kifedha. '

Dira ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania inatazamia kiwango kikubwa cha maendeleo ya rasilimali watu na inategemea nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Malengo ya Stanbic yanaendana na yale ya taifa huku ikijitahidi kutumia fursa zitokanazo na huduma za kifedha kuboresha maisha ya Watanzania. 


 Hivi karibuni, Benki ilipokea tuzo kwenye tuzo za “Banker Africa Awards” kwa kuwa ‘Benki bora kwa biashara ndogo ndogo na za kati’ nchini Tanzania. Huu ni mfano hai mwingine wenye kudhihirisha nia ya Stanbic katika kuleta maendeleo ya kweli kwenye biashara na ukuaji wa uchumi jumuishi nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...