Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Sheria na Katiba ya kumsimamisha, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga baada ya kukosa sifa za Uenyekiti wa Bodi hiyo. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia amesema kwamba hatua imefuatia Mkutano wa Juni 10 wa wanachama wa Yanga kusema bado unamtambua Yussuf Manji kama Mwenyekiti wao.

Karia amesema kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anatakiwa awe Mwenyekiti wa klabu ya Ligi Kuu, Sanga amepoteza sifa za kuwa kiongozi Mkuu wa bodi hiyo.

"Tulipokea barua Julai 12 kutoka klabu ya Yanga ikidai kuwa Sanga hatambuliki kama Mwenyekiti wa klabu hiyo, wao Yanga wanamtambua Yussuf Manji ndiye Mwenyekiti wa klabu hiyo na katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi unatakiwa Uwe Mwenyekiti wa klabu yako," amesema Karia 

Katika hatua nyingine, Karia amesema Kamati ya Utendaji imempitisha rasmi Wilfred Kidao kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kukaimu kwa muda mrefu.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kumvua uenyekiti wa bodi ya Ligi Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...