Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema kuwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya Juu pamoja na waajiri wanawajibu wakulipa mikopo ili kuweza kusomesha wengine.

Hayo aliyasema Mkurugenzi Msaidizi wa HESLB, Phidelis Joseph wakati wa maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika katika a viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mikopo ikirudishwa inasomesha wengine kutokana na wengine kuhitaji mikopo ya kuweza kupata elimu ya Juu.


Joseph amesema kuwa waajiri wakisha waajiri wafanyakazi katika taasisi, kampuni kupeleka majina bodi ili kuweza kuanza kukatwa mikopo na mwajiri na kupeleka bodi.

Amesema changamoto iliyopo ni waajiri kukata mkopo lakini hawapeleki bodi na wakati mwingine kupeleka kwa kuchelewa na kufanya bodi kuwa na utaratibu tozo kutokana na kuchelewa huko

Aidha amesema wamekuwa wakifanya kazi katoa elimu hiyo ikiwa ni watu kujua umuhimu wa kupata mikopo ya wanafunzio pamoja na urejeshaji kwa walionufaika na mkopo.

Amesema kuwa hakuna mtu anayeongezewa deni kinachofanyika ni thamani ya fedha kwa wakati husika katika urejeshaji wa mkopo.

“Nia ya Bodi ni kuona kila mtu aliyenufaika na mkopo anawajibu wa kulipa kwa wakati ili kusomesha wengine baada ya kukaa miaka miwili tangu alivyoohitimu” amesema Joseph
Mkurugenzi msaidizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Phidelis Joseph akizungumza na wananchi waliotembelea banda la bodi ya mikopo katika maonesho ya Vyuo Vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Afisa Ugawaji Mikopo wa HESLB , Vildenaunda Loshya akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Kibiti waliotembelea banda la bodi ya mikopo katika maonesho ya Vyuo Vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Baadhi ya maafisa wa Bodi wakiwapa maelekezo wananchi waliotembelea banda la bodi ya mikopo katika maonesho ya Vyuo Vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...