HOSPITALI ya Amana jijini Dar es Salaam , imekabidhiwa vitanda 10 vya kujifungulia wanawake vyenye thamani ya Sh. milioni 14 kama msaada uliotolewa na ubalozi wa China.

Vitanda hivyo vilikabidhiwa jana kwa Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk.  Meshack Shimwera na Waziri wa Madini, Angella Kairuki baada ya kuomba msaada katika Ubalozi huo na kukabidhiwa vitanda 36.

Akizungumza wakati akikabidhi viwanda hivyo, Waziri Kairuki amesema vitanda vitano walikabidhi hospitali ya vijibweni, Temeke vitanda sita na Amana vitanda 10.Amesema pia wataendelea kuvigawa katika Kituo cha Afya Sinza na Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala lengo likiwa ni  kupunguza idadi ya wanawake wanaojifungulia chini au kwenye vitanda vya kawaida.

“Msaada huu ni katika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini. "Leo nakabidhi vitanda 10 na nitajitahidi kuleta vitanda vingine ili kumaliza kabisa tatizo hili katika Mkoa wa Dar es Salaam  na kuhakikisha kila mwanamke anajifungua sehemu salama, " amesema Kairuki.

Naye Mganga Mkuu, Dk. Shimwera amesema vitanda hivyo vitafungwa kwenye wodi mpya ya kujifungulia wanawake na mahitaji yao yalikuwa ni vitanda 17.“Tunamshukuru Waziri Kairuki na ubalozi wa China, vitanda hivi tutavifunga kwenye wodi mpya hivyo vitasaidia akina mama wanaokuja kujifungua katika hospitali hii," amesema.

Pia amesena wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa magari ya kubebea wagonjwa baada ya waliyokuwa nayo saba kuyagawa kwenye vituo vya afya.Amesema kwa kuanzia wanahitaji magari matano ya kubebea wagonjwa pamoja na mashine ya CT-Scan na vifaa tiba kwenye chumba cha upasuaji na cha wagonjwa mahututi.


“Kutokana na kukosekana kwa mashine ya CT-Scan tunalazimika kupeleka wagonjwa 3,000 katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila lakini kama tungekuwa nazo tungeweza kuwatibu wenyewe," amesema Dk. Shimwera.
Waziri wa Madini,Angella Kairuki akimkabidhi Mganga mkuu wa hospital Amana,Dkt Meshack Shimwela vitanda 10 jijini Dar as Salaam. Picha na Emmanuel Massaka wa MMG.
Waziri wa Madini,Angella Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...