Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameutaka Uongozi wa mkoa wa Mbeya kuweka mpango wa kuyatumia maji ambayo yamechakatwa kutoka kiwanda cha soda cha pepsi cha SBC Mbeya. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Kiwanda Kipya cha Soda za Chupa za Plastiki cha Pepsi, SBC Mbeya. Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Mbeya, ameupongeza Uongozi wa SBC Mbeya kwa kuajiri Watanzania zaidi ya asilimia 90%.

“ Niliyoayaona yamenipa moyo na nimepata mafunzo pia nitakapokwenda kwenye viwanda vingine nini niwaelekeze cha kufanya” alisema Makamu wa Rais. Makamu wa Rais amepongeza kiwanda hicho kwa kuwa walipaji wazuri wa kodi na kwa wakati. Makamu wa Rais pia alipongeza mchango kwa jamii na michango mingine katika ngazi ya Kitaifa.

Mapema, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya SBC Tanzania Bw. Foti Nyirenda alimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki ktazalisha kreti 24,000 na pia Kiwanda cha Kuchakata maji taka ambapo kiwanda hicho kinatumia zaidi ya dola laki sita kwa ajili ya shughuli za kutunza na kuboresha mazingira. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil (kulia), Mkurugenzi Mkuu Bw. Avinash Jhah , Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Amos Makala na Meneja wa Kiwanda cha SBC Mbeya Mr. Sanam Mahambrey . (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya chupa ya plastiki wakati wa uzinduzi wa kiwanda kipya cha soda za chupa za plastiki katika kiwanda cha soda za Pepsi SBC Mbeya, kulia ni Mhandisi Mkuu wa Pepsi Tanzania Bw. Prabir Bhowmick na Msimamizi wa Mitambo Bw. Odestus Kabelenga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikitoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Ufunguzi wa kiwanda cha kuchakata maji taka SBC Mbeya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea maua kutoka kwa mtoto mwenye mahitaji maalum Amina Hawa kutoka Child Support Tanzania kama ishara ya kumkaribisha alipotembelea kiwanda cha Soda za Pepsi, SBC Mbeya. 

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...