Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Utawala Bora ni moja ya ahadi waliyoitoa kwa wananchi wakati wa kampeni.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika mkoa wa Songwe.
 “Lazima tunapofanya kazi zetu sheria zifuatwe, unapoacha kufuata sheria kwa sababu ya Matakwa binafsi, kwa sababu ya kunufaika wewe binafsi hili ni Tatizo hapa hapana utawala bora” 
alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais alisema Utawala bora usisukumwe tu upande wa Serikali unapaswa kupimwa kwenye ngazi zote mpaka za chini zikiwemo ngazi za Udiwani.Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Utawala bora ni pamoja na maendeleo ya Serikali yanapatikana.Makamu wa Rais amesema Serikali itajenga pamoja na kuboresha vituo vya Afya 9 katika mkoa wa Songwe ambapo wilaya ya Momba kutakuwa na vituo vitatu.

Mapema leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefungua kituo cha Afya cha Tunduma kilichofanyiwa maboresho na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 500 na ambacho kitahudumia wakazi zaidi ya elfu 80.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la  Kituo cha Afya cha Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi waTunduma  kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe. 

 Sehemu ya Umati wa wakazi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Tunduma mara baada ya kukifungua  ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Esther Luila mwenye umri wa miaka 7 mara baada ya kukifungua  kituo cha Afya Tunduma  ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na Wajasiriamali wa Wilaya ya Momba muda mfupi kabla hajahutubia kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma ikiwa siku ya tatu ya ziara yake mkoani Songwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...