NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu ,Charles Kabeho amemuagiza mtendaji mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na watendaji wake ,kwenda kufanya ukaguzi katika kiwanda cha Kuchi Jogoo kilichopo kata ya Visiga ,Kibaha mkoani Pwani ili kujiridhisha na kutoa kibali cha kuanza kuzalisha unga wa nafaka .

Amewataka wahakikishe wanatimiza agizo hilo mwisho July 26 mwaka huu na kupatiwa apatiwe majibu .Kabeho aliyasema hayo ,wakati mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukikabidhiwa mkoani Morogoro ukitokea Mkoani Pwani .

Alieleza endapo watachelea kufanya hivyo watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua .Alieleza wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi kiwandani hapo (july 19) alitoa siku saba kwa shirika hilo liwe tayari litimize agizo hilo .

Kabeho alisema ,haiwezekani kiwanda kikawa tayari kimekamilisha taratibu za uzalishaji na taratibu huku TBS ikawa kikwazo cha kushindwa kwenda kukagua na kutoa kibali baada ya ukaguzi.

"Mradi huo una gharama ya sh. milioni 812.7 ,ni mradi mkubwa na serikali inahimiza uwekezaji lakini ikitokea vikwazo ,inakwamisha adhma za serikali"Kiongozi huyo alisema kwamba ,kila mmoja atimize wajibu wake ili kuunga mkono juhudi za serikali pasipo kuweka vizuizi ambavyo vinaashiria suala la rushwa.

Hata hivyo Kabeho alisema ,viwanda vinasaidia kutoa ajira na kuinua pato la Taifa pamoja na uchumi .Aidha aliupongeza mkoa wa Pwani kwa kusheheni viwanda .
KIONGOZI wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu Charles Kabeho akimuaga mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo baada ya mwenge wa Uhuru kumaliza shughuli zake Mkoani Pwani na kuelekea Morogoro. 
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo alhaj Majid Mwanga (kulia ) akimkabidhi mwenge wa Uhuru mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo baada ya kutoka halmashauri ya Chalinze kisha kwenda kuukabidhi mkoa wa Morogoro.
MKUU wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto) akimkabidhi mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Stephen Kebwe (kulia ) eneo la mpakani mwa mikoa hiyo Bwawani.(picha na Mwamvua Mwinyi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...