Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

KAMPUNI ya Phimona Ltd inayojihusisha na ushauri wa biashara na mawasiliano kwa kushirkiana na wadau waliobobea kuhamasisha uwekezaji imetangaza kufanyika kwa Maonesho ya kukuza uwekezaji Tanzania(TIPEC).

Uamuzi huo una lengo la kuitambua , kutengenezea andiko na kuitangaza miradi kwa ajili ya uwekezaji hasa kwa kutambua eneo hilo halijanyiwa kazi kikamilifu. Wakati wa kutangaza maonesho hayo leo jijini Dar es Salaam mbali ya Phimona pia walikuwa wadau wengine wakiwamo TanTrade, TNBC, EPZA, TCCIA, NDC, TBC na TSN. 

Akizungumzi maonesho hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Phimona Rodgers Mbaga amesema kupitia maonesho hayo yanayofahamika kwa jina la TIPEC yatawaleta pamoja wenye miradi inayotafuta wawekezaji na wenye mitaji.

Ameongeza na kwa upande mwingine inawaleta wawekezaji na wenye mitaji kuja kukutana ana kwa ana na wenye miradi. Amesema lengo la maonesho hayo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kutangaza na kukuza uwekezaji wameamua kuaandaa maonesho ili kukuza miradi na kutafuta wawekezaji na wenye mitji.

"TIPEC 2018 itaitambua , kutengenezea andiko na kuitangaza miradi isiyopungua 300 .Ingawa sekta nyingine itatangazwa pia.Mkazo utakuwa kwa miradi ya viwanda na kilimo,"amesema. Mbaga amesema maonesho hayo yatafanyika kuanzia Novemba 14 hadi 16 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Said Tunda akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kufanyika kwa Maonesho makubwa ya kukuza Uwekezaji kuanzia Novemba 14-16, mwaka huu jijini kwa udhamini wa makampuni mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN Ltd). Kutoka kushoto kwake ni Mchambuzi wa Mazingira ya Biashara (TNBC), Kabenga Kaisi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko TSN, Goodluck Chuwa, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Phimona Ltd, Rodgers Mmbaga, Meneja Ukuzaji Biashara wa TANTRADE, Stephen Koberou na Meneja Huduma na Uanachama wa TCCIA, Fatuma Hamis.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...