Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesma wamekubaliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchin IGP Simon Sirro kuanza uchunguzi wa kina kuhusu mbwa aliyepotea.

Amefafanua mbwa aliyepotea anayo mafunzo yote ya kukamata wahalifu na anao uwezo mkubwa wa kukabiliana na matukio ya kihalifu kama askari,hivyo kupotea kwa mbwa huyo lazima uchunguzi huo ufanyike.

Lugola ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema tayari IGP Sirro amemueleza kuwa ameanza uchunguzi wa mbwa huyo na kwamba ni vema mjadala wa mbwa huyo ukasitishwa ili uchunguzi ufanyike.

Amefafanua katika ziara ambayo ameifanya hizo hivi karibuni katika vyombo vya ulinzi na usalama amepata nafasi ya kwenda katika kikosi cha mbwa na farasi."Mbwa na farasi walioko kwenye kikosi hicho 
wanatengewa fedha za chakuka na malazi.Mbwa na Farasi hao wanafanya kazi mbalimbali za ulinzi,"amesema Lugola.

Ameongeza maelezo ambayo aliyapata akiwa katika kikosi cha farasi na mbwa yanatofautiana na kila makabidhiano yanapofanyika kunakuwa na tofauti ya taarifa.Amesema katika kikosi hicho mbali ya farasi mbwa walikuwa sita lakini kwa sasa wamebaki watano na mmoja haieleweki yupo wapi.

"Nimekubaliana na IGP kufanya uchunguzi wa nini kimetokea hadi mbwa akapotea.Kwa kuwa jambo hilo linakwenda kuchunguzwa ni vema likaachwa sasa lifanyiwe uchunguzi," amesema Waziri Lugola.

Kwa siku kadhaa moja ya mjadala ni habari ya kupotea kwa mbwa mwenye mafunzo yote ya kipolisi na mbwa hao nao hujukana kama polisi na baada ya kubainika kupotea Lugola alitoa maagizo ya kutafutwa mbwa huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...