THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA YAWANOA VIONGOZI WANAWAKE DAR

Na said Mwishehe, Globu ya jamii 

SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeamua kuwanoa viongozi wanawake wa ngazi mbalimbali wakiwamo madiwani na wakuu wa Idara katika manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu maadili ya viongozi wa umma. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua semina ya mafunzo hayo Kamishina wa Sekratarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Harold Nsekela amesema yatatoa fursa kwa viongozi hao kufahamu sekretarieti kuanzia majukumu, kazi na wajibu walionao katika usimamizi wa maadili.

Amefafanua sababu za kutolewa kwa mafunzo yametokana na utafiti uliofanywa mwaka 2015 kupitia taaaisi yao ya Kukuza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu na kazi zinazotekelezwa na sekretarieti hiyo. "katika utafiti huo iliyokuwa unapoona ushiriki wa utoaji wa taarifa uliofanywa na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu ukiukwaji wa maadili miongoni mwa viongozi wa umma. 

"Matokeo yalionesha ni asilimia moja tu ya wanawake kwenye vijiji na mitaa walishiriki kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili, "amesema. 

Amesema hali hiyo ililazimu Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuandaa mafunzo hayo katika mikoa yote inayotekelezwa mradi huo ambayo ni Mtwara, Morogoro, Iringa na Dodoma. "Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uelewa viongozi wanawake katika mamlaka za Serikali za mitaa kuhusu maadili ya viongozi wa umma.