Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo leo ametembelea halmashauri ya wilaya ya Kibaha kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Katika Ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea kituo cha afya Mlandizi, ukarabati wa sekondari ya wasichana ya Ruvu, pamoja na uboreshaji wa Kituo cha afya cha Magindu ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.9 zimeshatolewa na serikali kufanikisha miradi hiyo. 

Akizungumza na wananchi wa Magindu waziri Jafo amewaambia wananchi hao kwamba serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli ni serikali ya vitendo sio ya kuahidi bila kutekeleza na kwamba kwa kizaramo "Sio ya walimila Dole". 

Jafo alitumia neno hilo la Lugha ya kizaramo kwa wakazi hao wa magindu ambao wengi wao ni wazaramo ili kuleta msisitizo.Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamood Abuu Jumaa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kiwaletea wananchi wa kibaha vijijini maendeleo ya kweli. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Kibaha vijijini Hamood Jumaa katika kituo cha afya Mlandizi mkoani Pwani.
Viongozi wakiwa Katika zoezi la ukaguzi wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri ya kibaha vijijini.
Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamood Abuu Jumaa akimkaribisha Waziri wa Nchi, Tamisemi Selemani Jafo kijijini Magindu ili aongee na wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...