THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Shahidi katika kesi ya kumiliki Mali zaidi ya kipato chake adai mtuhumiwa hakutamka magari 10 katika mali zake

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa TRA  Jennifer Mushi anayekabiliwa na kesi ya kumiliki magari 19 yenye thamani ya Sh. Mil 197 wakati wa uhakiki wa mali zake, walibaini kuwa na magari 10 ambayo hayakutamkwa.

Afisa Mchunguzi wa TRA, Tumaini Fadhir ameieleza hayo leo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akiongozwa na wakili wa serikali, Vital Peter amedai baada ya kupitia fumo za matamko mbali mbali ya Mali na madeni, walibaini magari zaidi ya kumi yaliyoonekana kwenye miliki za mshtakiwa yakiwa hayajatamkwa kwa mujibu wa taratibu.
"Nilifanya uchunguzi wa mali zote zinazohusika na zisizohusika na kibaini kuwa magali hayo hayakutamkwa ukichilia, magari hakuna mali zingine tulizobaini", amedai Tumaini.
Amedai kuwa, baada ya kubaini hayo, alitoa taarifa kwa menejimenti.

Katika ushahidi wake, Tumaini amedai  yeye ni mchunguzi wa ndani wa TRA, huku majukumu yake ni kuchunguza malalamiko ya watumishi,  kuhakiki mali za watumishi  zinazohusu matamko ya mali na madeni  kwa lengo la kuthibiti vitendo vya rushwa.

Aidha akihojiwa na wakili wa uetezi Furgence Masawe kama anamfahamu Jennifer, alijibu kuwa anamfahamu kwa sababu aliwahi kumchunguza. 

Pia aliulizwa kama anafamu idadi ya mali za Jennifer na thamani yake , Tumaini alijibu anafahamu. 

Pia aliulizwa Jennifer alianza kazi lini TRA, alijibu kuwa tangu mwaka 2011 lakini awali aliajiriwa katika sekta binafsi. 

Baada ya kutolewa ushahihidi huo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo  hadi August 16,2018.

Jenifer anakabiliwa na kosa la kumiliki magari 19 mali ambayo hailingani na kipato chake, anadaiwa aliyaingiza magari hayo nchini kutokea Japan yakiwa na thamani ya shilingi  Milioni 197,601, 207.