SERIKALI ya Tanzania imeomba wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali zikiwemo za Umoja wa Mataifa kuendelea kufanyakazi nayo kuhakikisha kwamba ajenda ya kimataifa ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030 inaendelea kutekelezwa nchini.
Hayo yalisemwa katika kikao cha kupewa taarifa ya utekelezaji wa malengo hayo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk Augustine Mahiga.
Aidha alisema serikali imetengeneza mikakati kadhaa ya kuwezesha kutekelezwa kwa malengo hayo ya dunia.
Alisema wakati Tanzania imekaza nia ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda suala linalosisitizwa katika SDG 9 ni muhimu na kwamba serikali ya Tanzania inataka kuendeleza ushirikiano huo ili malengo ya dunia yafikiwe pia nchini Tanzania.
Alisema Tanzania chini ya uongozi wa Rais John Magufuli inaendelea kutekeleza mpango wa maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa (SDGs) wenye lengo la kufikia ustawi kwa kila mkazi wa dunia hii.
Ili kutekeleza malengo hayo, mpango wa maendeleo wa miaka mitano umeingiza malengo ya SDGs.
“Kama nchi tangu tumeanza kutekeleza SDG kwenye mwaka 2016, tumechambua na kuingiza vipengele vya SDGs kwenye mipango mbalimbali ya kitaifa ikiwamo mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21 (FYDP II) na mpango wa tatu wa kukuza uchumi wa Zanzibar na kupunguza umaskini (MKUZA III)” alisema.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Augustine
Mahiga akitoa neno la ufunguzi wakati wa kikao cha kupewa taarifa ya
utekelezaji wa maendeleo endelevu kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akizungumza kwenye kikao cha
kupewa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo endelevu kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC)
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Profesa Adolf Mkenda akitoa neno la ukaribisho wakati wa kikao cha
kupewa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo endelevu kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC)
jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa maelezo mafupi kuhusu
mkutano wa mashauriano baina ya Serikali ya Tanzania na mashirika ya
Umoja wa Mataifa wakati wa kikao cha kupewa taarifa ya utekelezaji wa
maendeleo endelevu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Profesa Adolf Mkenda
Balozi
wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad akitoa maoni wakati wa
kikao cha kupewa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo endelevu
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Malawi nchini Tanzania, Hawa Ndilowe akizungumza wakati wa kikao cha
kupewa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo endelevu kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC)
jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akibadilishana mawazo
na mmoja wa wadau wa maendeleo wakati wa kikao cha kupewa taarifa ya
utekelezaji wa maendeleo endelevu kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es
Salaam
Baadhi
ya wadau wa maendeleo, viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na
Waheshimiwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini walioshiriki
kikao cha kupewa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo endelevu
kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam
Picha
ya pamoja ya viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo kutoka mashirika
mbalimbali na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini mara baada ya
kumalizika kwa kikao cha kupewa taarifa ya utekelezaji wa maendeleo
endelevu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...