WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa wakiwemo mawaziri na wabunge wawahamishe Watanzania kuendeleza utamaduni wao.

Ametoa wito huo leo (Jumatano, Julai 18, 2018) wakati akizungumza na wazee na wananchi wa Makunduchi mara baada ya kushuhudia maadhimisho ya sikukuu ya Mwaka-Kogwa yaliyofanyika Makunduchi, wilaya ya Kusini, mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

“Mawaziri wote, tuna dhamana ya kuwahamasisha Watanzania waendeleze utamaduni ili uwe ni jambo hai. Wabunge na wawakilishi tukiwa kwenye majukwaa, tusisitize Watanzania waendeleze utamaduni,” amesema.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zinasimamia uwepo wa utamaduni na zenyewe zinaongozwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo imelenga kuihamasisha  jamii kuuenzi,  kuulinda  na  kuudumisha utamaduni wa Mzanzibari na kushiriki katika uandaaji wa matamasha 50 ya utamaduni.

“Lazima utamaduni uendelezwe ndani na nje ya nchi na ni lazima tufanye jitihada tuwarithishe watoto utamaduni wetu. Kwa mfano, hapa Zanzibar mnalo tamasha la ZIFF, lile ni la kimataifa, vyombo vya muziki ni vya kisasa. Ni vema sasa, tukaangalia uwezekano wa kuwa na tamasha la huku chini ambalo litatumia ala za muziki za asili,” alisema.

Akizungumzia sherehe za Mwaka Kogwa, Waziri Mkuu alisema hii ni mara yake ya kwanza tangu azaliwe kuona watu wakichapana viboko si kwa ugomvi wala chuki, bali wakiwa na furaha.

“Mwaka Kogwa ni utamaduni wetu, pande zote za visiwani na zimekuwa zikifanyika kila mwaka lakini hivi sasa ni Makunduchi peke yake ambao mmeweza kuendeleza utamaduni huu, wengine wameacha kuadhimisha sherehe hizi,” amesema.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuhitimisha  Sherehe za Mwakakogwa, eneo la Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Sherehe za Mwakakongwa  zilizofanyika Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,  Hassan Khatib Hassan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria katika Sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika  Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika sala ya kumwombea Rais wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Idris Abdul Wakil kwenye kaburi la Rais huyo enero la Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018.  Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Sira Ubwa  Mwamboya, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja , Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja,  Hassan Khatib Hassan.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mohammed Abdulwakil ambaye ni Kaka wa Rais  wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Idris Abdul Wakil  Wakati  alipozulu kaburi la Rais huyo, eneo la Makunduchi, Zanzibar Julai 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa kofia na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Mwakakogwa, Mwalimu Makungu Mwita katika sherehe za Mwakakogwa zilizofanyika Makunduchi Zanzibar Julai 18, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...