Watumishi wa kada mpya ya afya wasiotaka kwenda kufanya kazi mikoani ndani ya siku 14 ambazo wameitwa kwa ajira mpya kinyume nah apo watakuwa wamejifuta kazi wenyewe, amesaema Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipotembeleaa Hospitali ya Rufaa mkoa Kigoma Maweni wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ya utoaji huduma za afya mkoani humo .

“Watumishi walioitwa kazini kwenye ajira mpya ya kada za afyana Wizara ya afya na kupangiwa Hospitali ya za Rufaa za Mikoa wanatakiwa wawe wameripoti vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu kuitwa kazini asiyefanya hivyo atakuwa amejifuta kazi mwenyewe.

"Serikali kupitia wizara hii imepanga kuweka utaratibu wa kuwafanya watumishi waliopo mikoani kupenda kufanya kazi kwenye vituo vyao vya kazi na wasitegee kupata uhamisho kwenda Dar es salaam", Waziri Ummy amesema, akiongeza kuwa Serikali haitaki kumuona Mwanamke mjamzito yeyote anapoteza Maisha kwa sababu ya kutimiza wajibu wake wa kuzaa hivyo wanaimarisha miundombinu ikiwemo kujenga wodi za mama wajawazito na watoto pamoja na vyumba vya upasuaji wa dharura wa kutoa mtoto tumboni kuhakikisha mjamzito anajifungua salama.

Katika kuboresha Afya za wananchi wa Kigoma Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 ya kukarabati miundombinu ikiwemo Wodi ya wagonjwa mahututi,Jengo la wagonjwa wan je (OPD), Wodi ya wagonjwa wa dharura na chumba cha upasuaji katika Hospitali hiyo ya Maweni.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Paul Chawote amesema kuwa amepiga hatua katika kupunguza vifo vya wajawazito mpaka kufikia vifo 34 ukilinganisha na miaka ya nyuma kwani walikuwa wanafanya vibaya.

Aidha Dkt. Chawote amesema kuwa idadi ya wajawazito wanaojifungulia kwenye katika vituo vya afya ni asilimia 78 na wajawazito wanaohudhuria kliniki ni asilimia 98 na upatikanaji wa dawa katika mkoa huo ni asilimia 95.

Mbali na hayo dkt. Chawote amesema kuwa mbali na mafaniko hayo kwenye huduma za afya bado Mkoa Kigoma unasumbuliwa na maambukizi ya Malaria ingawa upatikanaji wa dawa ,unyunyiziaji wa dawa kwenye mazalia ya mbu pamoja na kugawa vyandarua vyenye dawa vinafanyika kwa kaiasi kikubwa.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mama mzazi Bi. Leticia Lukurugu (23) mkazi wa Kigoma mara baada ya kujifungua salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni , kulia ni daktarin Bingwa wa watoto katika hospitali hiyo Dkt. Yakayashi Macrice wakati wa ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni , kulia ni daktarin Bingwa wa watoto katika hospitali hiyo Dkt. Yakayashi Macrice wakati wa ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya mpango wa Serikali juu ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi waliofika kupata matibabu katika salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni wakati wa ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiona wagonjwa na kukagua miundombinu ya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni wakati wa ziara yake mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...