WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameruhusu uingizaji wa vyavu za kuvulia samaki na dagaa kutoka nje ya nchi baada ya kubaini kuwa viwanda vya kuzalisha nyavu hizo vilivyopo nchini kushindwa kuhimili mahitaji ya soko la ndani na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wavuvi.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya operesheni Sangara 2018 jijini Dodoma, Waziri Mpina amemuagiza Katibu Mkuu- Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Rashid Tamatama kuhakikisha kuwa katika kipindi cha siku 14 awe amekamilisha kupitia maombi na kuruhusu uingizaji wa nyavu hizo kutoka nje ya nchi. Pia kuweka utaratibu ambao hautaathiri soko la viwanda vya ndani.

Mbali na hilo Waziri Mpina ameigiza wizara yake kuandaa mkakati wa kudhibiti upotevu wa mapato, usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi nchini ili kuondoa mianya yote ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuweka ulinzi thabiti wa rasilimali za uvuvi.

Pia ametaka Wizara hiyo kufanya mapitio ya mkakati wa ufugaji wa samaki kwenye maji, kufufua vituo vya kuzalisha vifaranga na kufanya tathmini ya uwekezaji wa sekta binafsi na kuainisha mahitaji ya sasa ili kuongeza uzalishaji utakaochangia kupunguza nguvu ya uvuvi kwenye maziwa na hivyo kutokomeza uvuvi haramu, kuongeza ajira na upatikanaji wa malighafi za viwanda nchini.

Akizungumzia matokeo ya operesheni Sangara 2018, Waziri Mpina alisema jumla ya watuhumiwa 3,998 walikamatwa kwa makosa mbalimbali na kutozwa faini na wengine kufikishwa Mahakamani,

nyavu haramu 575,152, makokoro 11,144 na kamba za kokoro zenye urefu wa mita 859,304 zilikamatwa na kuteketezwa kwa moto.Pia ndoano 1,910, 135 zisizoruhusiwa kisheria ziliharibiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...