Na Khadija Seif , globu ya jamii.

KAMPUNI ya kidigital ya huduma za kifedha (Branch) imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuanza kwake.

Ambapo imejikita katika sekta ya teknolojia-fedha kwa kutangaza kujiunga na mfumo wa huduma mpya na Airtel jijini Dar es salam.

Mwanzilishi wa Kampuni hiyo Branch, Ofisa Mtendaji Mkuu Matthew Flannery ameeleza dhumuni la kuanzishwa kwa Kampuni hiyo ni kutokana na uhitaji mkubwa wa kifedha ili kuendeshea biashara mbalimbali kwa wateja ambao wanakosa mikopo ya kufanikisha mahitaji yao, hivyo basi huduma hiyo itawapa fursa za kupata fedha haraka zaidi.

Flannery amesema zaidi ya asilimia 75 ya wateja wanatumia mikopo ya Branch kuwasaidia kuanzisha na kukuza biashara zao au kutimiza mahitaji mengine ya kifedha. 

Akizungumzaa na wanahabari Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Afrika Masharki Dan Karuga amefafanua kuwa Branch ni kampuni ya kipekee inayotoa huduma vyenye viwango vya hali ya juu katika huduma za kifedha,kupitia mpango wao wa kutoa mikopo hususani kwa makundi ya watu wasiofikiwa kiurahisi.

Na kufanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wateja mbalimbali nchini kote. Karuga ameeleza lengo la huduma hiyo ni kutoa fursa kwa wananchi kupata mikopo haraka kupitia simu za mikononi ,na watumiaji wanaweza kutumia smartphone zenye uwezo wa Internet kujipatia mkopo kuanzia Sh. 50,000 hadi Sh.100,000.

" Inachukua sekunde chache kutoka kutuma maombi hadi kukubaliwa kwa ombi la mkopo,pia haihitaji kuonana ana kwa ana na mtoa huduma kwa njia ya vikao."Utaratibu mrefu wenye sura simu,dhamana ya kujaza fomu za karatasi. Pia tangu ianze huduma zake Tanzania,Branch imekwishatoa mikopo ya zaidi ya Sh.billioni 12 na mikopo zaidi ya 400,000,"amesema Karuga

Amesema kuwa Branch international, inatarajia kutoa mikopo ya Sh. Billioni 570 na kutoa mikopo mipya zaidi ya laki tano amesema Karuga.

Nae mmoja wa watumiaji wa hudumu ya Branch, Mtangazaji mahiri wa Radio ya EFM Dina Marios alikiri wazi urahisi wa kuitumia huduma hiyo popote na kwa wakati wowote ule kujipatia mkopo ambao unaweza ukatumia kuanzisha biashara yako.

Hivyo amewahimiza Watanzania kujitokeza kutumia huduma hiyo ili kujiongezea kipato kwa namna moja ama nyingine na hatimae kujikwamua kiuchumi.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Branch Afrika Masharki, Dan Karuga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar kuhusu kampuni hiyo kuadhimisha mwaka mmoja na mikakati yake mbalimbali ikiwemo na kujitanua kibiashara zaidi nchini Tanzania
Pichani kushoto ni Mwanzilishi wa Kampuni Branch, Ofisa Mtendaji Mkuu Matthew Flannery akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar kuhusu kampuni hiyo kuadhmisha mwaka mmoja ,dhumuni la kuanzishwa kwa Kampuni hiyo hasa kwa nchini Tanzania pamoja na mikakati mingine ya kujitanua zaidi kibiashara
Mmoja wa watumiaji wa hudumu ya Branch, Mtangazaji mahiri wa Radio ya EFM Dina Marios akitoa ushuhuda mbele ya Waandishi wa Habari,namna kampuni hiyo inavyoweza kuwanufaisha Watanzania,kupitia mikopo inayotelewa iliyo na masharti nafuu kabisa.
Baadhi ya Wanahabari wakifutilia yaliyokuwa yakijir ukumbini humo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...