Na Benny Mwaipaja, Kasulu, Kigoma

Naibu Waziri wa Fefha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Wakala wa majengo Tanzania-TBA, kutekeleza kwa wakati mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma ili kuiepusha Serikali kutumia fedha nyingi kutokana na kuongezeka kwa gharama za miradi husika kunakotokana na ucheleweshwaji huo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendelelo ya ujenzi wa Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu zinazojengwa na Serikali kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 na kutaarifiwa kuwa TBA, wamechelewa kuanza ujenzi huo kwa zaidi ya miezi 12 wakati fedha zilikwisha tolewa na Serikali.

Aliishauri TBA kujipanga kukamilisha miradi inayopewa na Serikali kwa wakati kwa kuongeza idadi ya wataalam wanaoweza kusimamia miradi mingi inayotekelezwa na wakala huo.

"Pesa zipo, Serikali haiwezi kuanza kutekeleza mradi wowote kama hakuna pesa, ni jukumu lenu kama TBA kuhakikisha mnawezesha mradi huu ukamilike kwa wakati ili tupate thamani halisi ya fedha za mradi" alisisitiza Dkt. KijajiDkt. Kijaji alitoa wito kwa wakazi wa Mji wa Kasulu na Kigoma kwa ujumla kuchangamkia fursa za ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao kwani lengo la Serikali kujenga miradi hiyo ni kuwawezesha pia wananchi kiuchumi.

Hatua hiyo inafuatia taarifa iliyotolewa na Mhandisi wa ujenzi wa Jengo hilo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Bw. Abubakari Basuka, kwamba miongoni mwa changamoto inayoukabili mradi huo ni ukosefu wa mafundi mchundo na vibarua ambapo imeelezwa kuwa vijana wengi katika eneo la mradi hawajitumi kufanyakazi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akiwasili kukagua mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Mkoani Kigoma, katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Bi. Fatina Hussein Laay, na kulia ni Mhandisi wa mradi huo Bw. Abubakari Basuka.
Mhandisi wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Bw. Abubakari Basuka (aliyevaa kofia) akisoma taarifa fupi ya Mradi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wa tatu Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Bi. Fatina Hussein Laay (kushoto), akieleza umuhimu wa kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Ofisi za Halmashauri yake ya Mji kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) kwa kuwa ofisi zinazotumika sasa hazikidhi mahitaji, wa pili kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA, Bw. Elijah Mwandumbya.
Muonekano wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mji Mkoani Kigoma litakalo gharimu takribani Sh. Bilioni 2.5.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...