Na Rhoda James- Mtwara

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jana tarehe 10 Agosti, 2018 amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa Mtambo wa kusambaza Gesi Asilia majumbani mkoani Mtwara. Waziri Kalemani, amefanya zoezi hilo leo katika shule ya Ufundi ya Mtwara mara baada ya kuzidua MW4 za umeme katika kituo cha Umeme cha Mtwara.

Waziri Kalemani alisema kuwa, ujenzi wa mtambo huu umegharimu jumla ya billioni 1.5 kwa ajili ya kuwapelekea watumiaji wa awali wasiopungua 150 ambao bada ya miezi mitatu wataanza kutumia gesi hiyo majumbani. Aliongeza kuwa matumizi ya gesi asilia ni madogo sana yaani ni kama hayapo, kwa kuwa wananchi wengi wanatumia kuni na mkaa kwa wengi kuliko gesi.

“Sasa mtugi wa gesi ni takriban shilingi 55,000/- lakini ukitumia gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani itakuwa shilingi 25,000/- na utatumia kwa mwezi mzima hivyo ni nafuu kwa mwananchi wa Tanzania,” alisema Wazari Kalemani.

Mwezi mei tulianza matumizi ya gesi manyumbani lakini leo tumeanza matumiz ya gesi asilia katika mkoa wa Mtwara. “hayawi hayawi yamekuwa,” alisema Waziri Kalemani. Aidha, Waziri Kalemani aliendelea kueleza kuwa, Kuna magari zaidi ya 100 wanatumia gesi asilia jijini Dar es Salaam, hivyo kuazia mwezi Machi mwaka kesho (2019) tutaanza usanifu ili magari ya mkoa wa Mtwara nayo yaanze kutumia gesi asilia.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa nne kushoto) mara bada ya kuzidua mradi wa ujenzi wa mtambo wa usambazaji wa gesi asilia majumbani mkoani Mtwara. Wengine katika picha ni viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakiwa pamoja na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (wa tatu kulia) na wa kwanza kulia Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) akifatilia jambo kwenye ramani (haipo pichani) ya jinsi gesi hiyo itakavyo sambazwa majumbani. 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali serikalini pamoja na wabunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (mwenye kilemba) na wa nne kushoto ni Mbunge wa jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...