Ujenzi wa daraja la Kikamba wilayani Songwe linalounganisha Mkoa wa Songwe na Katavi ukiendelea daraja hilo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Songwe Mhe. Philipo Mulugo alipokagua ujenzi wa daraja la Kikamba wilayani Songwe, daraja hilo linaunganisha Mkoa wa Songwe na Katavi.
 Muonekano wa barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39 ambayo ujenzi wake unaendelea, barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa KM 293 inayounganisha kwa njia fupi mkoa wa Mbeya na mikoa ya Singida na Tabora.

SERIKALI imesema haitamwongezea mkataba mkandarasi China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara ya Chunya –Makongolosi kwa kiwango cha lami muda wake utakapomalizika.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amesema muda wa miezi 27 aliyopewa kujenga barabara hiyo yenye urefu wa  KM 39 unatosha na hivyo ni jukumu lake kuhakikisha kuwa anakuwa na vifaa na wafanyakazi wa kutosha wakati wote.

“Mkishindwa kukamilisha barabara hii kwa wakati hamtapata tena kazi hapa nchini kwani mtakuwa mmeshindwa kazi kwa kukiuka mkataba na kuiongezea Serikali gharama”, amesema Mhe. Kwandikwa.

Naye Kaimu meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Mbeya Mhandisi Selemani Lawena amesema barabara ya Chunya –Makongolosi ni sehemu ya barabara ya Mbeya-Rungwa yenye urefu wa KM 293 ambayo inaunganisha kwa njia fupi mkoa wa Mbeya na mikoa ya Singida na Tabora.
“Barabara hii ikikamilika itafungua uchumi wa mikoa ya Mbeya na Songwe na kuhuisha shughuli za kilimo,mifugo, uchimbaji madini na ufugaji nyuki na hivyo kuongeza fursa za maendeleo kwa jamii na serikali kwa ujumla”, amesema mhandisi Lawena.

Mhandisi lawena amesema sehemu ya Mbeya- Chunya KM 72 imekamilika na ujenzi wa Chunya –Makongolosi KM 39 unatarajiwa kukamilika Januari 2020.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua ujenzi wa barabara ya mchepuo ya Iwambi-Mbalizi KM 6.5 jijini Mbeya  ambayo itatumiwa na magari madogo ili kupunguza msongamano na ajali katika mlima Mbalizi na kusisitiza umuhimu wa wadau wote wa usafiri kushirikiana ili kupunguza ajali na hivyo kulinda maisha na mali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...