ZIARA
ya Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani
(UNHCR),Volker Turk imehitimishwa jijini Dar es salaam huku akihimiza
kuwa kila mkimbizi ana haki ya kuamua aidha kurejea nchini kwake au la.
Turk
amekuwa nchini kwa siku nne kuanzia Agosti 13 mpaka Agosti 16 Agosti
2018 ,Turk amehitimisha ziara yake kwa kukutana na wanahabari jijini Dar
es salaam, katika ziara hiyo aliambatana na Mratibu wa tume Afrika
Valentin Tapsob na Mratibu wa wakimbizi (kanda) kutoka Burundi bi.
Catherine Wiesner.
Lengo
la ziara hiyo ya Kamishina kutoka UNHCR ilikuwa ni kufanya majadiliano
yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na masuluhisho kwa
zaidi ya wakimbizi 34o,000 na wale wanaoomba hifadhi (asylum seekers)
nchini.Imeelezwa
kuwa idadi kubwa ya wakimbizi waliopo nchini wanatoka katika nchi za
Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ambapo asilimia 87 wanaishi
katika kambi 3 zilizopo Mkoani Kigoma.
Kamishina
Turk pia ametembelea kambi ya wakimbizi Nduta ambapo alishuhudia
mchakato wa kuwarejesha makwao wakimbizi kutoka Burundi na hadi sasa
zaidi ya wakimbizi 42,000 wamerejea nchini Burundi.
"
Haki ya wakimbizi lazima iheshimiwe katika kuamua kurejea nchini mwao
au la" amesema Turk na kuongeza kuwa maamuzi hayo yaangalie taarifa
iliyotolewa bila kulazimishwa aidha arejee au la.Pia
wawakilishi kutoka nchini Burundi wamekutana na Kamishina Turk na
kueleza kuwa idadi ya wakimbizi imefikia 400,000 hadi kufikia Julai 31
mwaka huu.
Aidha
imesemwa kuwa hali ya wakimbizi kutoka Burundi imekua chini zaidi
duniani katika kupokea misaada ya kibinadamu, UNHCR na washirika wengine
walipokea asilimia 12 ya dola milioni 391 za kimarekani pekee kwa mwaka
2018 na mwaka 2017 asilimia 21 ya misaada ilipokelewa kwa ajili ya
wakimbizi kutoka Burundi.
Kutokana
na hali hiyo Turk ameiomba jumuiya ya kimataifa kuangalia hali hiyo ya
kusahaulika kwa wakimbizi katika kupatiwa misaada ya kibinaadamu.Katika
ziara hiyo ambayo Kamishina Turk alikutana na mamlaka za serikali,
wakuu wa balozi, wafadhili na wadau mbalimbali nchini ameaidiwa kuwa
Tanzania itahakikisha maamuzi ya wakimbizi katika kurejea nchini kwao
yataheshimiwa.
Kamishina
msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker
Turk akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana
jijini Dar kuhusiana na ziara yake ya siku nne,lengo ya ziara hiyo
ilikuwa ni kufanya majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu
changamoto na masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 340,000 na wale
wanaoomba hifadhi (asylum seekers) nchini.
Kamishina
msaidizi (ulinzi) kutoka shirika la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker
Turk akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jana jijini Dar kuhusiana
na ziara yake ya siku nne,lengo ya ziara hiyo ilikuwa ni kufanya
majadiliano yaliyohusisha serikali na wadau kuhusu changamoto na
masuluhisho kwa zaidi ya wakimbizi 340,000 na wale wanaoomba hifadhi
(asylum seekers) nchini.Pichani kushoto ni Mratibu wa tume ya Afrika
Valentin Tapsob,Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
kuhudumia Wakimbizi Tanzania (UNHCR), Chansa Kapaya na kulia ni Mratibu
wa wakimbizi (kanda) kutoka Burundi,Catherine Wiesner.
Baadhi
ya Wanahabari wakimsikiliza Kamishina msaidizi (ulinzi) kutoka shirika
la wakimbizi Duniani (UNHCR),Volker Turk alipokuwa akizungumza nao
kuhusu ziara yake ya siku nne aliyoifanya nchini Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...