Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James amewataka watanzania kuchangamkia fursa ya kununua matrekta yaliyopo katika kiwanda cha kuunganisha matrekta ambacho kinamilikiwa na Serikali kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Amesema kuwa matrekta hayo yanaubora wa hali ya juu na kuwahakikishia wananchi watakaoyanunua matrekta hayo kutokuwa na hofu kwani uingizwaji wake Serikali inahusika moja kwa moja.Katibu James aliyasema hayo Kibaha mkoani Pwani wakati akikabidhi matrekta kumi kwa Chuo cha kilimo Sokoine (SUA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi I littles na Rais Dkt.John Magufuli baada ya kufanya ziara chuoni hapo .

Alifafanua rais alipofanya ziara chuoni hapo alihaidi mambo mawili la kutoa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ahadi ambayo tayari imetekelezwa na jana amekamilisha ahadi ya kukabidhi matrekta hayo." Ninawataka kwenda kutumia vizuri matrekta haya na kuyafanyia matengenezo iwapo yatahitaji matengenezo kwani sisi watanzania hatuna utaratibu wakutuza vitu hata kama tukiona vimeharibika."alisema James.

Nakuongeza kuwa" Sisi kama serikali tunachombo maalum cha kufatilia fedha na ahadi zote ambazo zinatekelezwa ,hivyo hata matrekta haya tutafatilia kuona yanatumikaje na iwapo mkitumia vizuri na hata kama.mkiomba zingine tutawapa"alisema James.Akizungumzia taasisi hizo za fedha hususani Mfuko wa Pembejeo wa Serikali pamoja na Benki kuwaeleza wananchi kuwa wanafedha kwa ajili ya kilimo ili waweze kuchangamkia fursa hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Doto James akikata utepe pamoja na viongozi wengine wakati wa kukabidhi matrekta kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) cha Mkoani Morogoro kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo. Matrekta hayo yametolewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa chuo hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Doto James akikata wakishangilia mara baada ya kukata utepe pamoja na viongozi wengine wakati wa kukabidhi matrekta kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo. Matrekta hayo yametolewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa chuo hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Doto James akijaribu kuwasha moja ya Matrekta yaliyokabidhiwa kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo. Matrekta hayo yametolewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa chuo hicho.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Doto James akizungumza wakati wa kukabidhi matrekta kwa Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye kiwanda cha TEMCO Kibaha mkoani Pwani leo.
Dk. Leonard Akwilapo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia akizungumza katika hafla hiyo kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Doto James . KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...