Na Editha Karlo,Blobu ya Jamii Kagera.

MKUU wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wanakagera kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya ya kikazi aliyoanza ili kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake.

Gaguti ameyasema hayo leo kwenye ukumbi wa halmashauri ya Bukoba baada ya kukabidhiwa ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Meja Jenerali Salum Kijuu na kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu.

Alisema nafasi yake ni kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wake kwa wanakagera ili kuhakikisha Mkoa wa Kagera unasonga mbele."Ni wajibu wangu kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wangu na nina imani kubwa tutashirikiana na viongozi wenzangu na nitatoa ushirikiano wakati wowote nipo tayari"alisema Mkuu huyo wa Kagera

Gaguti alisema Mkoa wa Kagera ni Mkoa ambao upo mpakani na unapakana na nchi karibia tatu hivyo aliwataka wananchi wa Mkoa huo kutumia fursa hiyo kuuza mazao ili kuufanya Mkoa kuwa wa viwanda na wenye neema.

Mkuu wa Wilaya ya Kywerwa Rashid Mwaimu baada ya kuapishwa alisema kuwa atakwenda kusimamia mapato katika Wilaya yake na kuhakikisha yanaongezeka ili shuhuri za maendeleo ndani ya Wilaya hiyo zifanyike vizuri.

"Najua nina majukumu makubwa na kazi yangu ni kutatua matatizo ya wananchi ili Wilaya yetu iweze kufanya vizuri katika sekta za miundombinu,afya na Elimu"alisema.
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimkabidhi nyaraka za ofisi mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti kwenye ofisi za halmashauri ya Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Maico Gaguti akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu katika ukumbi wa halmashauri ya Bukoba.

Baadhi ya viongozi wa chama ,Serikali na kamati ya Ulinzi Mkoa wa Kagera wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kwa Mkuu wa Mkoa na kuapishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...