Na.khadija seif ,Globu ya jamii.

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John pombe Magufuli kukuza sekta ya viwanda Taasisi ya ki_uanachama ya African Forestry (AF) ikishirikiana na Taasisi ya Uendelezaji Misitu Tanzania (FDT) ya Mkoani Iringa wameanzisha jukwaa la kuwasaidia wawekezaji wa sekta ya kilimo cha miti nchini Tanzania,na kuwapatia taarifa na elimu ya kilimo cha miti kwa njia ya mtandao ili kuongeza chachu ya uwekezaji katika sekta ya misitu.

Aidha akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya ki_uanachama ya African Forestry (AF) Francis Rwebegora amesema Misitu hiyo ina manufaa kwa jamii kwani misitu inafaida kwani baadhi ya mazao ya misitu ni pamoja na mbao zinazotumika katika sekta ya ujenzi ,viwanda vya kutengeneza samani,magogo yanayotumika katika viwanda vya karatasi ,nguzo za umeme na simu .

Rwebegora amefafanua zaidi faida nyingine za misitu ni pamoja na udhibiti wa ongezeko la joto kwani miti hutumia hewa_ukaa,kusanisi chakula chake, utunzaji wa vyanzo vya maji ,na faida nyingine nyingi za ki_ikolojia.

Mratibu wa biashara na masoko Taasisi ya Uendelezaji misitu nchini(FDT) Emmanuel sangalah amesema wakulima watapata mafunzo stahiki kuhusu kilimo cha miti kuanzia kuandaa shamba ,upatikanaji wa mbegu bora, utunzaji wa shamba,masoko,bei na ushauri wa kitaalam kea kuongeza pato la Taifa.

Ameeleza hatua jinsi ya kujiunga na huduma hiyo kupitia simu ya kiganjani nakutembelea tovuti ya www.mitibiashara na hakuna malipo yoyote ya kujiunga na jukwaa hilo na kutoa wito kwa wakulima kujiunga ili waweze kunufaika na mazao bora.
Mkurugenzi wa Taasisi ya African Forestry (AF) Francis Rwebegora akizungumzaa na wanahabari jijini Dar es salaam leo katika ufunguzi wa   huduma ya Mitibiashara kimtandao kwa ajili ya wakulima kupata elimu jinsi ya kuandaa mashamba yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...