Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa J.K Nyerere uliopo Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MOCu) kwa ajili ya kufungua mkutano wa Tano wa chama hicho.

Na Dixon Busagaga,Moshi.

CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) kimeiomba serikali kutunga sera ya uwepo wa eneo rafiki la kulelea au kunyonyeshea watoto katika sehemu za Kazi pamoja na kuunda chombo cha kusimamia utekelezwaji wa uwepo wa sera ya unaynyasaji wa kijinsia katika taaasisi za elimu ya juu nchini.

Mbali na ombi hilo THTU pia kimewasilisha ombo kwa serikali la kuundwa Vyombo vya kufuatilia waajiri ambao hawazingatii maagizo ya sera zinazotungwa na serikali ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi sambamba na uwepo wa muundo wa utumishi kwa wafanyakazi waendeshaji katika taasisi za umma za elimu ya juu nchini.
Hayo yalibainishwa wakati wa mkutano mkuu wa tano wa chama hicho unaofanyika kwa siku mbili katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ukishirikisha zaidi ya wanawake 80 kutoka vyuo vikuu 36,vitatu vikiwa ni vya binafsi na 33 vya serikali . 
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.

Katika risala yao kwa mgeni rasmi ,iliyosomwa na katibu wa THTU,Amina Mdidi ,wanawake hao walisema THTU imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kutokuwepo kwa mwongozo wa mishahara au bodi ya kusimamamia na kudhibiti malipo ya watumishi kwa vyuo binafsi.

“Changamoto nyingine zinazootukabili ni baadhi ya taasisi kutolipa nauli za likizo kwa enza wa wafanyakazi wanawake (Mume) na watoto chini ya miaka mitano na ukosefu wa vituo rafiki kwa malezi ya watoto wachanga”alisema Mdidi.

Katika hatua nyingine ,Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania kilitoa ripoti ya utafiti juu ya utekelezaji wa sera ya maendeleo ya mwananmke na jinsia ya mwaka 2000 katika taasisi za elimu ya juu Tanzania ikionyesha aslimia 80 ya taasisi hizo zilionyesha kutokuwepo kwa masuala ya jinsia katika mpango mkakati wa taasisi.

Baadhi ya Wajumbe wakiwa katika mkutano huo.

Akisooma utafiti huo ,Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake (THTU) taifa Salma Fundi alisema asilimia 80 ya taasisi hazikuonyesha uwepo wa mafunzo kwa wanafunzi au wafanyakazi kuhusiana na masuala ya jinsia.

“Asilimia 70 ya taasisi hazina sera ya unyanyasaji wa kijinsia ambazo ni muhimu katika kupunguza ubaguzi wa kijinsia na ukatili huku asiliamia 60 ya washiriki walikuwa na mtazamo hasi juu ya sera ya jinsia kwa kuamini ni sera inayomhusu mwanamke tu”alisema Fundi.

Katika hotuba yake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo,Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu,Stella Ikupa alisema THTU kwa muda mfupi kimekuwa chama kinachotoa chachu ya maendeleo na amani ndani ya taasisi za elimu ya juu Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...