Na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi maonesho ya Nane Nane Kanda ya kati ambayo yanaenda sawa na mashindano ya Nane ya Mifugo kitaifa yanayofanyika jijini Dodoma.

Ulega amefungua mashindano ya Mifugo ambayo yalianza mwaka 2011 na huwa yanafanyika Agosti 5  ya kila mwaka mkoani Dodoma na hujumuisha ng'ombe wa maziwa na nyama walioboreshwa pamoja na Mbuzi wa asili.Akizungumza jana Ulega amesema kuwa lengo kuu la mashindano hayo ni kutambua umuhimu na mchango wa rasmilimali za mifugo ya asili katika kuendeleza sekta ya mifugo nchini.

Aidha amesema kuwa mchakato huo linalenga kutambua juhudi na maarifa wanayotumia wafugaji wa mifugo ili kufuga kwa tija na hatimaye kuvutia wafugaji wengi na kuiga na kuingia kwenye ufugaji wenye tija kwa taifa.Ulega amesisitaza kuwa sekta ya mifugo ni moja ya Sekta muhimu zinazochangia kupunguza umaskini wa wananchi na kukuza uchumi wa nchi kwani ni mhimili katika kuendeleza viwanda kama ilivyoainishwa katika mpango kabambe wa Mifugo Tanzania.

Hata hivyo ametoa maagizo kwa wafugaji na wadau mbalimbali kuunda na kuimarisha vikundi na vyama vya ushiriki ili kuongeza kasi ya uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao ya mifugo na hatimaye kufikia malengo na kauli mbiu ya Nane Nane 2018 isomekayo ''WEKEZA''.Aidha Ulega ameagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha utekelezaji wa mfumo wa utoaji kinga mbalimbali za magonjwa ya mifugo uwe ni lazima kwa wafugaji wote nchi.

Pia Ulega amesema wafugaji pamoja na wafanyabiasha  hawaruhusiwi kuhamisha au kusafirisha mifugo pamoja  mazao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali.Hivyo imesababisha maeneo ya mipakani mwa nchi yetu imeshamiri biashara haramu za mifugo na mazao yake zisizo rasmi na amewataka watendaji kusimamia sheria kwa kushirikiana na wadau ili kutatua changamoto ya utoroshaji wa rasilimali za mifugo yetu na mazao yake.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia viatu katika banda la Magereza vinavyotegenezwa kwa bidhaa ya ngozi katika maonesho ya Nane Nane Nane ndani ya viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge wakitembelea banda la wajasiriamali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia samaki aina ya kamongo aliekaushwa katika banda la wajasiriamali katika maonesho ya Nane Nane yanayo fanyika ndani ya viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...