Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) akitembelea maeneo
mbalimbali katika kiwanda cha Kuchakata Madini ya Graphite cha
GodMwanga Gems Ltd. Wa kwanza kulia ni Mmiliki wa kiwanda hicho
Godlisten Mwanga na wa kwanza kuli kwa waziri ni Kaimu Mkuu wa Wilaya
ya Simanjiro, Tumaini Magesa.
Mmiliki wa kampuni ya God Mwanga Gems Ltd.Godlisten (kulia) Mwanga
akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki madini ya Grahite ambayo
tayari yamechakatwa.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) akipita katika maeneo
mbalimbali ya kiwanda cha God Mwanga Gems Ltd kuona namna shughuli
mbalimbali za uchakataji wa madini ya Kinywe zinavyofanyika.
Na Asteria Muhozya, Simanjiro
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema anaona fahari kutokana na
uwekezaji wa Kiwanda cha Kuchakata madini ya Kinywe (Graphite)
uliofanywa na Kampuni ya wazawa ya GOD Mwanga Gems Ltd iliyopo
Kata ya Endiamtu, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.
Waziri Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 2 Agosti, alipotembelea
kiwanda hicho kwa lengo la kujionea shughuli zinazofanywa na kiwandani
hapo.
Amesema Serikali imekuwa ikihamasisha waombaji wa leseni za madini
kuwekeza katika maeneo mbalimbali hivyo, jambo lililofanywa na kiwanda
hicho ikiwemo malengo ya kiwanda husika kufungua viwanda vingine
katika mikoa ya Tanga na Manyara ni jambo la kujivunia na fahari kwa
Tanzania.
“Nimefurahishwa sana namna kampuni hii inavyofanya kazi. Serikali kupitia
wizara yangu imekuwa ikihamasisha uwekezaji. Tuko tayari kuwasimamia
na kuwasaidia katika hili. Tunataka kutengeneza ajira zaidi, kukuza uchumi
kupitia madini lakini pia serikali kupata kodi,” amesisitiza Kairuki.
Akijibu ombi la kampuni hiyo kupata kibali cha kuuza madini hayo nje,
Waziri Kairuki ameahidi kampuni hiyo kuwa mara baada ya taratibu za
utoaji vibali kukamilika Wizara kupitia Tume ya Madini itatoa kibali kwa
kampuni husika iendelee na taratibu zake za kuuzwa nje ya nchi madini
hayo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...