WATENDAJI wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) wametakiwa kwenda walipo wananchi ambao hawako katika sekta isiyo rasmi ili wawaze kutoa elimu ambayo itawezesha kujiunga na hatimaye wanufaike na mafao mbalimbali yanayotolewa na Mfuko huo. 
 Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga mara baada ya kutembelea banda la NSSF wakati wa kilele cha maonesho ya nane nane kwa kanda ya Magharibi yalifanyika mjini Tabora. 
 Alisema mpango huo unachama wa hiari na sekta binafsi unatakiwa kuwafikia wananchi wengi ambao wamejiari wenyewe ili nao wajiunge kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni kupitia michango ambayo watakuwa wakichangia kila mwezi wakati wakiwa na nguvu. 
 Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga alisema jambo hilo ni zuri kwani tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961 hakuna Mfuko ambapo uliweza kumjali mtu asiye katika sekta isiyo rasmi na kuongeza kuwa ni jukumu la Watumishi wa NSSF kwenda kwao ili wawahimize waweze kuchangamkia fursa hiyo ambayo ni msaada kwao. 
 “Msisubiri wananchi wawafuate bali mnatakiwa kuwafuata walipo katika shughuli zao na kuwaelimisha ili hatimaye wengi wajiunge”alisema. 
 Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema Mfuko huo umekuja na mpango ambao umjali Mtanzania wa kipato cha chini naye kupata kiunua mgongo akichangia kwa miaka isiyopungua 15 kama alivyo mtumishi mwingine. 
 Alisema mpango huo unawahusisha watu kama vile mamalishe, boda boda, muuza karanga na wengine wote ambao walikuwa hawana mifuko ya kuchangia sasa wanatakiwa kujiunga na NSSF ili hatimaye kunufaika wakiwa wazee. 
 Naye Meneja wa NSSF Mkoa wa Tabora Nour Aziz aliwataka watu ambao sio waajiriwa katika sekta rasmi kuchangamkia kwani NSSF inawakinga na majanga ya kiuchumi na kijamii kwa kutoa mafao kulingana na taratibu zilizowekwa na hivyo kumwezesha kufanyakazi bila hofu kwa kuwa wanamwezesha kujenga maisha yao ya sasa na baadae. 
 Alisema kuwa kupitia michango ya shilingi 20,000 ambazo wanachama atatoa kila mwezi, akifikisha miezi mitatu na kuendelea atapata Kadi ya Matibabu ambayo itamwezesha yeye na watoto wake wanne na wenza kupata matibabu na huku akiba yake ikiwa palepale.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akitoa maelezo mafupi jana kwa mgeni wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga wakati walipotembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) kwenye kilele cha maonesho ya nane nane kwa Kanda ya Magharibi ambayo yalifanyika mjini Tabora.
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Mkoani Tabora Victor Mbesigwe (kulia) akitoa maelezo kwa wananchi juu ya uanachama wa hiari na jinsi mwananchi kutoka sekta binafsi navyoweza kujiunga. Alitoa amaelezo hayo leo wakati wa kilele cha maonyesho ya nane nane ambapo kwa kanda ya magharibi yalifanyika mkoani Tabora.
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) Mkoani Tabora Victor Mbesigwe (kushoto) akitoa maelezo kwa mwananchi Ngunda Shija (kulia) juu ya uanachama wa hiari na jinsi mwananchi kutoka sekta binafsi navyoweza kujiunga. Alitoa amaelezo hayo leo wakati wa kilele cha maonyesho ya nane nane ambapo kwa kanda ya magharibi yalifanyika mkoani Tabora.
Mtumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tabora Ester Mng'omba (kushoto) akimsaidia Dereva wa Boda Boda kujaza fomu ya kuwa wanachama wa hiari mara baada ya kutembelea banda hilo jana wakati wa kilele cha maonyesho ya nane nane ambapo kwa kanda ya magharibi yalifanyika mkoani Tabora.
Picha na Tiganya Vincent

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...