Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelewa ofisini kwake na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia na Mwenyekiti wa Michezo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wamefanya mazungumzo ya kuimarisha sekta ya Michezo.

Miongoni mwa mambo waliyozungumzia ni Suala la heshima iliyopata Tanzania kuwa mwenyeji wa Michuano ya Mashindano makubwa ya michezo kwa Jeshi la Polisi katika nchi za mashariki na Kati zikihusisha Nchi Saba ambapo tayari michuano hiyo imefunguliwa rasmi siku ya Jana na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Aidha wamezungumzia maandalizi ya mashindano makubwa ya SECAFA Cuf kwaajili ya michuano ya AFCON yakihusisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayotaraji kufanyika August 11 Mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa yakijumuisha mataifa 10 Afrika.

RC Makonda amesema michuano yote hiyo itafanyika Jijini Dar es salaam na kwakuwa inahusisha ugeni kutoka mataifa mbalimbali itatoa fursa kwa wananchi wa Dar es salaam hususani wenye hotel, vyakula, usafiri na wafanyabiashara kupata kipato kupitia mashinano hayo.

Kwa upande wake Rais wa TFF Wallance Karia amempongeza RC Makonda kwa jitiada za kuinua sekta ya michezo kupitia ujenzi wa uwanja wa Bandari ambapo amesema wameamua kumuomba ushirikiano kwakuwa wanaamini uwezo ukubwa alionao kwenye kusimamia jambo na kufanikisha.
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusiana na michuano ya Vijana ya AFCON itakayofanyika mwakani hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya ujio wa Rais wa TFF Wallace Karia ofisini kwake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...