Na Woinde Shizza, Manyara

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Elexander Mnyeti amezindua ligi ya Chemchem inayoshirikisha timu 20, yenye lengo la kupiga vita ujangili ambayo itagharimu zaidi ya sh 35 milioni.

Akizungumza juzi katika uzinduzi huo katika viwanja vya mdori, wilayani Babati, Mnyeti ambaye aliwakilishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Augustine Senga amezitaka timu zitakazoshiriki kucheza kwa nidhamu ili kufikia malengo ya ligi hiyo.

Mnyeti amesema ligi hiyo pia inapaswa kutumika katika kuibua vipaji kwa wachezaji chipukizi ili kuweza kusajiliwa katika timu za ligi kuu."Najua hapa kuna vipaji hivyo michezo hii ni fursa ya kujulikana zaidi na hivyo kuwa sehemu ya kutoa ajira kwa vijana na kujenga afya"amesema

Katibu wa mashindano hayo John Bura amesema jumla ya timu 20 za soka zinatarajia kushiriki michuano hiyo na kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa nne."Pia kutakuwa na ligi ya wanawake ambayo itashirikisha timu tatu na washindi watapewa zawadi,"amesema

Amesema katika michuano hiyo mchezaji bora,mfungaji bora na timu yenye nidhamu, watapata zawadi na hivyo, akawataka kucheza soka la kuvutia.Awali Meneja wa Chemchem ambao ni wadhamini wa ligi hiyo, Kanali mstaafu Leonard Werema amesema taasisi hiyo inayofanya shughuli za utalii katika eneo hilo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori(WMA) ya Burunge.

Na kwamba inataka ligi hiyo, kusaidia kutoa elimu ya kupiga vita ujangili na uhifadhi.Werema amesema Chemchem imegharamia zaidi ya Sh.milioni 35 katika michuano hiyo, ikiwepo kuandaa uwanja na majengo kuandaa zawadi, imetoa vifaa vya michezo kwa timu zote 23 na gharama nyingi za waamuzi na waratibu wa michuano hiyo chama cha soka wilaya ya Babati.

Katika mchezo wa ufunguzi, mabingwa watetezi, Mdori FC walipata ushindi wa magori 3-2 dhidi ya timu ya City Boys katika mchezo mkali uliochezwa kiwanja cha mdori.
 MKUU wa Mkoa wa Manyara, Elexander Mnyeti pichani juu na chini akisalimiana na baadhi ya wachezaji wakati akizindua  ligi ya Chemchem inayoshirikisha timu 20, yenye lengo la kupiga vita ujangili ambayo itagharimu zaidi ya sh 35 milioni.Akizungumza juzi katika uzinduzi huo katika viwanja vya mdori, wilayani Babati, Mnyeti ambaye aliwakilishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Augustine Senga amezitaka timu zitakazoshiriki kucheza kwa nidhamu ili kufikia malengo ya ligi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...