Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekabidhi Fedha za fidia kwa Wananchi waliopisha Ujenzi wa Karantini ya Mifugo katika eneo la Nziwengi katika Jimbo la Gando liliomo ndani ya Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Fedha hizo zilizotolewa na Serikali na Kukabidhiwa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi zimelengwa kwa Wakulima 40 waliokuwa wakiendesha shughuli zao za Kilimo na Mifugo katika eneohilo linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa Hekta 60.9.

Akikabidhi fedha hizo kwa Wakulima hao, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema subra iliyofanywa na Wakulima hao wa Jimbo la Gando hatimae imeleta neema itakayowaenea Wananchi wa jimbo hilo hasa wakati huu wa kuelekea kwenye Siku Kuu ya Iddi El – Hajj.

Balozi Seif aliwaasa na kuwakumbusha Wakulima na Wananchi hao wa Gando wawe makini katika matumizi ya fedha walizokabidhiwa kuzilenga kwenye uanzishaji wa shughuli za Kilimo walizokuwa wakizifanya katika maeneo mengine.

“ Nimefarajika kushuhudia kitendo hichi cha ulipaji wa fidia kwa wakulima wa Gando nikiwa kama Mwakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Kazi hii”. Alisema Balozi Seif.Alieleza kwamba Serikali Kuu katika kushajiisha Kilimo Nchini imeanza kutoa Miche ya Minazi bure kuwapa Wakulima katika maeneo mbali mbali kama inavyofanywa kwa Miche ya Mikarafuu.

Akitoa Taarifa fupi ya ujenzi wa Karantini ya Mifugo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Nd. Ahmad Kassim Haji alisema eneo la Gando lilikuwa likikumbwa na miripuko ya Maradhi mengi yanayotokana na uingizwaji wa Mifugo kiholela.

Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Makame Haji Kushoto akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ramani ya Ujenzi wa Nyumba za Wahanga wa Mvua za Masika zilizopita zinazotaka kujengwa katika Kijiji cha Tumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba,
Balozi Seif akimkabidhi Mkulima Bibi Safia Hamad Khamis wa Kijiji cha Gando Hundi ya Fedha kwa ajili ya Fidia ya mazao yao ili kupisha Ujenzi wa Karantini ya Midugo kwenye eneo la Nziwengi.Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis Othman na kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Kilimo Mh. Rashid Ali Juma na Naibu Wake Dr. Makame Ali Ussi.
Balozi Seif akimkabidhi Hundi Bwana Ali Khamis Ali kwa ajili ya ulipwaji wa fidia ya mazao yao ili kupisha Ujenzi wa Karantini ya Midugo kwenye eneo la Nziwengi.Picha na – OMPR – ZNZ.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...