Na Stella Kalinga, Simiyu

Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini.

Mhe. Mkapa amesema hayo katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

“Ninachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.

Aidha, amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia usalama wa chakula katika kaya zao.Mkapa pia amesema Serikali ina mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kutoka tani 121,000 mwaka 2016/2018 hadi kufikia tani milioni moja mwaka 2020.

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ametangaza rasmi kuwa Maonesho ya Nane nane Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo hadi mwaka 2020 yatafanyika kanda mpya Kanda ya Ziwa Mashariki katika Uwanja wa Nyakabindi Bariadi, huku akisisitiza kuwa maonesho hayo yafanyike Kimataifa kwa kushirikisha nchi jirani zinazoizunguka Tanzania.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akizungumza na wananchi katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa Simiyu mwaka 2018, katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akiwapungia mkono wananchi (hawapo pichani), katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 , katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akikagua Banda la Jeshi la Magereza wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi., katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu, katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Mtaalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Kilimo akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa kuhusu Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki kupitia Vizimba.
Mkulima kutoka Wilaya ya Maswa akipokea zawadi yake ya fedha taslimu katika Kilele cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kwa kuwa mkulima bora kutoka Wilayani Maswa.KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...