WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wabadilike na watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kulalamika.

Amesema kama kuna changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasilina na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Agosti 8, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Nandagala.Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa, alisema vijana wanatakiwa kujitambua na kuiunga mkono Serikali kwa kufanyakazi kwa bidii.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa pamoja katika kubuni shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo litawakwamua kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama.

PiaWaziri Mkuu aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani humo, Agosti 8.2018 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimshuhudia aliyekua Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Waitara, akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi, katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018
Aliyekua Mwenyekiti wa Kata ya Nandagala Jafari Omari (katikati), akikabidhi kadi yake ya CHADEMA kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa, Agosti 8.2018 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Nandagala Wilayani Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Wilayani hapo, Agosti 8.2018 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa kata ya Nandagala wakati akiwasili katika uwanja wa zahanati ya kijiji cha Nandagala kwa jailli ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Agosti 8.2018.Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...